• HABARI MPYA

    Tuesday, June 02, 2015

    BLATTER AJIUZULU URAIS FIFA BAADA YA KUBANWA NA FBI KASHFA YA RUSHWA

    MTIKISIKO, Rais wa FIFA Sepp Blatter ametangaaa nia yake ya kujiuzulu kufuatia kashfa ya rushwa.
    Katika taarifa iliyotolewa leo makao makuu ya FIFA mjini Zurich, Uswisi, Blatter amesema anaondoka baada ya miaka 17 kama mtu wa nguvu katika soka. Akizungumza leo, Blatter amesema; "Nitaendelea na nafasi yangu FIFA hadi wakati ujao. Uchaguzi mpya utafanyika Mexico,". 
    Blatter kwa sasa yuko chini ya uchunguzi mkali wa FBI kama bodi hiyo ya soka ilihusika na rushwa. 
    Idara ya Sheria ya Marekani imesema dola za Kimarekani Milioni 10 walipewa Wajumbe wa zamani wa FIFA, Jack Warner na Chuck Blazer kutoka akaunti ya FIFA katika benki ya Uswisi mwaka 2008.
    Gazeti la New York Times limesema kwamba malipo hayo yalifanywa na Katibu Mkuu, Jerome Valcke. Valcke amekana madai hayo na Mkuu wa Idara ya Vyombo vya Habari ya FIFA, Delia Fischer amesema ni Julio Grondona aliyefanya malipo hayo.
    Baadaye ikagundulika Valcke alikuwa anafahamu kuhusu malipo hayo. FIFA imeitisha Mkutano baadaye na Blatter anajiandaa kuhudhuria.Sepp Blatter has announced he will stand down as FIFA president - though will continue in the role until an 'extraordinary congress' can be called to vote in a successor

    Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu Urais wa FIFA, ingawa ataendelea kuwa madarakani hadi Mkutano Mkuu utakapoitishwa kumchagua mrithi wake

    Malipo hayo ambayo yanafanyiwa uchunguzi na FBI, inadaiwa fedha hizo walilipwa Makamu wa Rais wa zamani wa FIFA, Jack Warner na Msaidizi wake Chuck Blazer kama malipo yao kwa kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenye wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010.
    Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amekanusha nchi yake kuhonga ili kupata uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia.  
    Blatter amekiri tuhuma hizo hizo zimechafua kila kitu katika miaka yake 17 ya kuongoza soka kwa ufanisi wa hali ya juu na babu huyo wa umri wa miaka 79, ambaye alishinda tena uchaguzi wa FIFA Ijumaa kwa mara ya tano licha ya tuhuma hizo, amekanusha kuwa muhusika wa sakata hilo ambaye hakutajwa jina.
    "Hakika siyo mimi," Blatter alisema katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumamosi. Warner, ni miongoni mwa Maofisa 14 wa FIFA waliofunguliwa mashitaka na Idara ya Sheria ya Marekani Jumatano iliyopita kwa tuhuma za rushwa ya zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 150.  
    Warner alitoka jela mjini Trinidad and Tobago Alhamisi na mara moja akamgeukia Blatter akihoji kwa nini naye hachunguzwi.  
    This letter addressed to Jerome Valcke was published by SABC News on Tuesday morning
    Barua hii iliyoelekezwa kwa Jerome Valcke imechapishwa na na Shirika la Habari la SABC leo asubuhi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BLATTER AJIUZULU URAIS FIFA BAADA YA KUBANWA NA FBI KASHFA YA RUSHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top