• HABARI MPYA

    Monday, October 15, 2012

    AZAM TAYARI WAPO MBEYA TANGU JANA

    Azam FC

    Na Mahmoud Zubeiry
    AZAM FC tayari wapo mjini Mbeya tangu jana saa 1:00 usiku, kwa ajili ya yao ya Jumatano, dhidi ya wenyeji Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
    Azam waliondoka Morogoro jana asubuhi baada ya mechi yao ya juzi dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri na watafanya mazoezi kuanzia leo, ili kuzoea hali ya hewa ya mji huo.
    Mbeya ni kati ya vituo ambavyo vinawaogopesha vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam, Simba na Yanga kutokana na imani kwamba Prisons haifungiki kwenye Uwanja wake.
    Sababu kubwa ni ubovu wa Uwanja wa Sokoine, ambao wenyewe Prisons wameuzoea na wanaujulia, wakati timu nyingine hupata tabu mno.
    Kati ya vigogo hao watatu, ambao wanafukuzana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, Azam inakuwa timu ya pili kwenda Mbeya, baada ya Yanga iliyolazimishwa sare ya bila kufungana na Wajelajela hao kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi hiyo.
    Simba imeanzia Dar es Salaam kucheza na Prisons, Septemba 29, mwaka huu katika mechi ambayo walishinda kwa taabu mabao 2-1 na sasa watarudiana na Wajelajela hao mjini Mbeya katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.   
    Mikoa mingine tishio ni Kanda ya Ziwa, ambako Azam tayari imekwishamaliza na kukusanya pointi nne baa ya kuifunga 1-0 Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Yanga pia imemaliza deni la Kanda ya Ziwa, ikiambulia pointi tatu, baada ya kufungwa 1-0 na Kagera na kushinda 3-1 dhidi ya Toto. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM TAYARI WAPO MBEYA TANGU JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top