• HABARI MPYA

    Friday, October 19, 2012

    AZAM WAPO CHAMAZI TANGU JANA USIKU TAYARI KWA KIPUTE NA JKT RUVU JUMAPILI

    Kikosi cha Azam

    Na Mahmoud Zubeiry
    AZAM FC imerejea Dar es Salaam jana majira ya saa 1:00 ikitokea Mbeya, ambako juzi ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Azam sasa wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wao ujao, Jumatano dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex, Dar es Salaam. 
    Pamoja na sare hiyo, Azam wamelalamikia uchezeshaji mbaya wa marefa wa mechi hiyo, kwamba uliwapokonya ushindi.
    Azam FC wanadai refa alikataa mabao yao mawili yaliyofungwa na Abdi Kassim ‘Babbi’ na penalti ya wazi, baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ kuangushwa kwenye eneo la hatari
    Wanadai bao la kwanza, refa alilolikataa ulikuwa ni mkwaju wa mbali wa Abdi Kassim ambao ulitinga nyavuni, kabla ya kurudi uwanjani na refa licha ya kuona kuwa lilikuwa ni bao halali, bado akaamua kukataa
    Wanadai baadaye, Sure Boy alifanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na kwa mshangao wa wengi, wakiwemo viongozi na wachezaji wa Prisons ambao walishashika vichwa, refa akapeta na mpira kuendelea
    Zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika, Azam FC wanadai walipata adhabu ndogo na Abdi Kassim aliupiga mpira ule na kutinga nyavuni, lakini kwa mara nyingine tena refa akakataa bao kwa madai kuwa kabla ya kufunga, Babbi alikuwa ameotea.
    Baada ya ‘kufanyiwa dhuluma’ hiyo, Azam wanaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa wana pointi 17, baada ya kucheza mechi sana, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wapo kileleni kwa pointi zao 18 na wamecheza mechi nane.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM WAPO CHAMAZI TANGU JANA USIKU TAYARI KWA KIPUTE NA JKT RUVU JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top