• HABARI MPYA

    Friday, June 08, 2012

    ERIKSSON AMTETEA HODGSON KUMTEMA RIO


     6 Juni, 2012 - Saa 11:48 GMT
    Kocha wa timu ya England Roy Hodgson

    KOCHA mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya England Sven-Goran Eriksson anasema wanaomshtumu kocha wa sasa Roy Hodgson kwa kutomchagua Rio Ferdinand kwenye timu wana nia ya kumchafulia jina.
    Ferdinand hakuwepo kwenye kikosi cha kwanza kilichotajwa na kocha Roy Hodgson na wakati Gary Cahill alipopata jeraha, kocha huyo alimuita Martin Kelly mwenye umri wa miaka 22.
    " Kumchagua Kelly inaonekana kumemponza," Eriksson alisema. "kwa kuwa amechagua wachezaji sita wa Liverpool, Roy sasa anaandamwa.
    " Najua Roy atakabiliana na hali hiyo bila wasiwasi wowote."
    Hodgson, ambaye tayari ameiongoza timu hiyo kupata ushindi katika mechi mbili za kirafiki tangu kuchukua uongozi wa timu ya England mwezi uliopita, amesisitiza kuwa kuachwa nje kwa Ferdinand ni kwa sababu za kimchezo wala siyo vinginevyo.
    Hata hivyo wengi wanaamini ni kwa nia ya kuepuka matatizo kati yake na John Terry, ambaye anatarajiwa kufika mahakamani mwezi ujao kwa tuhuma za kumrushia maneno ya ubaguzi wa rangi mdogo wake Ferdinand, Anton, tuhuma ambazo nahodha huyo wa Chelsea,Terry anakanusha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ERIKSSON AMTETEA HODGSON KUMTEMA RIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top