Ugiriki
VIKOSI VYA LEO |
POLAND Szczesny Piszczek, Wasilewski, Perquis, Boenisch Murawski, Polanski Blaszczykowski, Obraniak, Rybus Lewandowski |
UGIRIKI
Chalkias Torosidis, P'thopoulos, P'dopoulos, Holebas Karagounis, Katsouranis, ManiatisSalpingidis, Gekas, Samaras |
WENYEJI washirika wa Euro wa 2012, Poland hawana majeruhi kuelekea mechi yao ya ufunguzi wa michuano hiyo na kocha Franciszek Smuda anatarajiwa kushusha kikosi kile kile kilichocheza mechi mbili zilizopita za kirafiki.
Hiyo inamaanisha, wachezaji wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek, Jakob Blaszczykowski na Robert Lewandowski wataanza, wakati Rafal Murawski na Eugen Polanski watasimama katika safu ya kiungo wakati 'Tai Mweupe' akifungua kampeni za michuano hiyo.
Ugiriki nao wapo kamili na leo wanatarajiwa kutumia mfumo wa 4-3-3 dhidi ya wenyeji hao. Vasilis Torosidis yuko shakani kucheza kufuatia kuumia goti dhidi ya Slovenia wiki iliyopita, lakini beki huyo wa kulia amekuwa akifanya mazoezi siku za karibuni.
Sotiris Ninis pia ni majeruhi,licha ya kinda huyon wa miaka 21 kuelezwa kwamba yuko fiti na atacheza. Mshambuliaji huyo wa Panathinaikos, anaweza kuanzia kwenye benchi katika mechi ya leo na Dimitris Salpingidis anatarajiwa kucheza upande wa kulia katika safu ya washambuliaji watatu.
JE WAJUA? |
Poland ni mwenyeji mshiriki wa michuano hii ya Euro, wakishirikiana na Ukraine - hii ikiwa mara ya kwanza kwao kuandaa michuano hiyo mikubwa.
- Tai Mweupe ilifuzu kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Ulaya mwaka 2008, lakini ikashika mkia kwenye kundi lake, kwa kuambulia pointi moja.
- Poland imekutana na Ugiriki mara 15 na imewanyanyasa wapinzani wao hao wa Ulaya, ikiwafunga mechi 10, kutoka sare mbili na kufungwa tatu.
- Vijana wa Smuda wameweka rekodi ya taifa ya kushinda mechi tano mfululizo, wakicheza dakika 461 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa, tangu wafungwe na 2-1 na Hungary, Novemba 15, 2011.
- Ugiriki ilifuzu Euro 2012 kwa kuongoza Kundi F, ikimaliza na pointi 24 na haikufungwa hata mechi moja, ikifuatiwa na Croatia na Israel.
- Kuna wachezaji watatu waliokujwamo kwenye kikosi cha ubingwa cha Euro 2004-katika fainali hizi za Poland na Ukraine: Giorgos Karagounis, Kostas Katsouranis (pichani kulia) na Kostas Chalkias.
- Ugiriki bado haijaweza kuepuka vipigo vya Poland, na katika mechi nane wamefungwa zote, wakifunga mabao manne tu, wakati wao wamefungwa 22.
- Karagounis ameichezea mechi 117 Ugiriki, anazidiwa tatu tu na Theodoros Zagorakis, ambaye anashikilia rekodi ya taifa.
0 comments:
Post a Comment