![]() |
Wachezaji wa Azam |
WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC leo wanaanza rasmi mazoezi kwenye Uwanja wao, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame.
Kulingana na programu ya maandalizi, Azam FC wataanza mazoezi leo asubuhi, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi maalum kwa mashindano hayo yatakayofanyika mwezi ujao mjini Dar es Salaam.
tayari wachezaji wa Azam kutoka nje ya Tanzania wamewasili mapema wiki hii na wamepatiwa makazi.
Usajili kwa wachezaji Azam ulikwishamalizika kabla ya wachezaji kwenda likizo, hivyo wachezaji wote waliosajiliwa wataanza mazoezi isipokuwa wale walioko kwenye timu zao za taifa, Tanzania, Uganda na Zanzibar, ambazo zipo kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa wikiendi hii.
Programu ya maandalizi ya Kombe la Kagame, itamalizika siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo na yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Maandalizi kwa ajili ya VPL yatahusisha pia ziara ya nje ya nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema nchi hiyo itatajwa baadaye.
Wachezaji wapya kiikosini Azam msimu huu ni kiungo Mkenya George ‘Blackberry’ Odhiambo na kipa Deogratius Munishi kutoka Mtibwa Sugar, wakati Aishi Salum, Jackson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga, wamepandishwa kutoka akademi ya Azam.
Kikosi kamili cha Azam FC kinaundwa; na makipa, Mwadini Ally, Deo Munishi ‘Dida’ Aishi Salum na Jackson Wandwi, mabeki wa Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samir Haji Nuhu, Luckson Kakolaki, Said Mourad, Joseph Owino na Aggrey Morris.
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadalla, Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche, Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati washambuliaji ni Gaudence Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’.
Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza Kombe la Kagame, baada ya kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu. Katika Kombe la Kagame mwaka huu, wenyeji Bara wataingiza timu tatu, Yanga ambao ni mabingwa watetezi, wakati Simba na Azam wanaingia kwa nafasi za uwakilishi.
0 comments:
Post a Comment