Timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars leo inatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Ethiopia katika mchezo wa marudiano kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Katika mchezo wa kwanza, Twiga Stars ilifungwa mabao 2-1 na kwenye mchezo wa leo, ili ikate tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara pili mfululizo, inahitaji ushindi wa 1-0. Kocha wa Twiga, Charles Boniface Mkwasa amesema mabinti wako vizuri na ana matumaini ya ushindi katika mchezo wa leo. Mkwasa amewataka Watanzania, hususan wanawake kujitokeza kwa wingi jioni ya leo kuishangilia timu yao hiyo, ili kuwapa hamasa wachezaji waweze kufanya vizuri na Tanzania ishiriki tena fainali za Afrika. Kila la heri Twiga Stars. Mungu ibariki Tanzania. AMIIN. |
0 comments:
Post a Comment