Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya 

CHELSEA KUNG'OA KITASA CHA NGUVU CHA UFARANSA

KLABU ya Chelsea iko tayari kumnasa beki wa kulia wa kimataifa wa Ufaransa, Mathieu Debuchy mwenye umri wa miaka 26 kutoka klabu ya Lille mbele ya pua za Newcastle.
KIUNGO aliye katika wakati mgumu, Alberto Aquilani hataruhusiwa kutia saini mkataba wake wa Liverpool, lakini Joe Coe anatarajiwa kuweka rekodi kwa kurejea kwa Wekundu hao.
Thiago Alcantara
Thiago Alcantara
KLABU ya Manchester United, inamfuatilia kiungo wa Barcelona, Thiago Alcantara, mwenye umri wa miaka 21, na bado ina malengo ya kumsajili nyota wa  Tottenham, Luka Modric.
KLABU ya Everton inajaribu kumsajili Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 26, ambaye amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaong'ara kwenye Euro 2012 hadi sasa akiwa ameifungia mabao matatu Croatia.
KLABU ya Manchester City matumaini ya kumnasa beki Thiago Silva kutoka AC Milan yalipungua hadi sifuri, baada ya klabu hiyo ya Italia kukataa ifa ya pauni Milioni 37 kwa ajili ya mchezaji huyo wa zamani wa PSG, mwenye umri wa miaka 27.
MSHAMBULIAJI alyetemwa Manchester united, Michael Owen, mwenye umri wa  miaka 32, ameamua kujiunga na Stoke City licha ya kwnza na Everton inamtaka pia mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na Newcastle .
KLABU ya Arsenal inayongoza mbio za kuwania saini ya mcheaji wa Real Madrid, Joselu mwenye umri wa miaka 22.
KLABU bingwa ya Ulaya, Chelsea iliweka mezani dau la pauni Milioni 20 kuinasa saini ya  nyota wa Fiorentina, Stevan Jovetic, mwenye umri wa miaka 22, lakini likapigwa chini na klabu yake.

POLANDA KUKOSA KITASA CHAKE CHA MAANA LEO EURO 2012...

BEKI wa Poland, Damien Perquis, mwenye umri wa miaka 28, ataukolsa mchezo wa lep dhidi ya Jamhuri ya Czech Republic katika Euro 2012 kutokana na kuwa majeruhi.
HODDLE AMLILIA REDKNAPP
KOCHA wa zamani wa England, Glenn Hoddle amesikitishwa na kufukuzwa kwa kocha Harry Redknapp katika klabu ya Tottenham na kusema kwamba uamuzi huo, haukutokana na sababu za kisoka.
KLABU ya Birmingham inaye Roy Keane katika orodha ya makocha wanne wanaowafikiriia - kuwapa kazi .
Roy Keane
Roy Keane on Birmingham's short-list
KIUNGO mwenyer majeruho sugu, Owen Hargreaves, mwenye umri wa miaka 31, anafikiria kustaafu kabisa soka.