![]() |
Majeruhi wakiwa nje ya mazoezi |
![]() |
Nge wa Gambia wakipasha Karume jioni hii |
![]() |
Benchi la Ufundi |
![]() |
Bin Zubeiry kushoto akiagana na kocha Machini baada ya mahojiano Karume |
![]() |
Wachezaji wa Gambia wakitoka uwanjani baada ya mazoezi |
![]() |
Kiungo wa Gambia, Saihou Gassama (18), anayechezea Real Zaragoza B ya Hispania
|
KOCHA Mkuu wa Nge wa Gambia, Mtaliano, Luciano Machini
amesema mechi ya Jumapili dhidi ya wenyeji Tanzania, Taifa Stars ya Kundi C
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, itakuwa ngumu
kwa sababu wapinzani wao ni wazuri.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY katika mazoezi ya timu
hiyo jioni ya leo Uwanja wa karume, Machini aliyechukua nafasi ya aliyekuwa
bosi wake, Peter Bonu Johnson, Mei mwaka huu, amesema kwamba Taifa Stars ni
wazuri na wana kasi uwanjani, hivyo mechi hiyo hata wachezaji wake wanajua
itakuwa ngumu.
Alisema wao walicheza vizuri dhidi ya Morocco kwenye mechi
yao ya kwanza, lakini wanaingia kwenye mechi ngumu na wenyeji Jumamosi.
Machini aliwaongoza vijana wake kwa mazoezi mepesi jioni ya
leo Uwanja wa Karume na inaonekana kama ana majeruhi wasiopungua watatu, ingawa
benchi la ufundi la timu hiyo kwa ujumla limefanya siri juu ya hali za afya za
wachezaji wao.
Nge wa Gambia waliotoka sare ya 1-1 nyumbani na Morocco
kwenye mechi ya kwanza Jumamosi, waliwasili nchini jana saa 5.30 usiku kwa
ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars, iliyofungwa 2-0
na Ivory Coast katika mechi ya kwanza ya Kundi hilo Jumamosi mjini Abidjan,
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 31 wakiwemo wachezaji 22
unaongozwa na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo wan chi
hiyo, Malang Jassey.
Viongozi wengine ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha
Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa
makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr
Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso,
Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju,
Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay,
Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa,
Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
Baada ya mazoezi ya leo, Nge hao, watafanya tena mazoezi yao
kesho asubuhi Uwanja wa Karume na jioni Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment