Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

LUCA MODRIC SAFI MAN UNITED

KIUNGO wa Tottenham, Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, yuko njiani kuelekea Manchester United, kutokana na Sir Alex Ferguson kupandisha ofa ya pauni Milioni 25, hadi Milioni 30 ili kuinasa saini ya nyota huyo.
KLABU ya Manchester United ina matumaini ya kumsajili beki wa kushoto wa Valencia, Jordi Alba, mwenye umri wa miaka 23, ingawa inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Barcelona, ambayo imepania kukamilisha usajili wa kisiki hicho wiki hii.
KLABU ya Inter Milan inataka kumsajili beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov mwenye umri wa miaka 26.
Aleksandar Kolarov
Aleksandar Kolarov.
MLINDA mlango wa Birmingham, Ben Foster, mwenye umri wa miaka 29, anawaniwa kwa nguvu zote na Queen's Park Rangers katika jitihada zao za kusaka kipa mpya namba moja.
KLABU ya Tottenham Hotspur imeripotiwa kukubali dili la kumsajili kinda wa Nottingham Forest, mwenye umri wa miaka 18, beki wa kati Jamaal Lascelles  , ikiipiku Arsenal, ambayo nayo ilikuwa inamtaka.
KLABU ya Newcastle imejitosa kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji aliyetemwa Chelsea, mshambuliaji  Salomon Kalou, mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa yuko huru kuondoka baada ya kuipa klabu yake, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

UHOLANZI WAPEWA YA NYANI

KIKOSI cha Uholanzi kimekumbana na adha ya ubaguzi- wachezaji wake weusi wakifanyiwa ishara ya nyani wakati wa mazoezi ya wazi ya kujiandaa na Euro 2012 mjini Krakow, Poland - siku moja kabla ya England kupanga zoezi kama hilo.
KIUNGO Niko Kranjcar ameelezea furaha yake baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Dynamo Kiev kufuatia kusema kwamba kuwa kwake Tottenham ilikuwa majuto tupu.