SENEGAL imeondolewa kwenye fainali zijazo za Mataifa ya Afrika baada ya vurugu kubwa zilizofanywa na mashabiki wake zilizosababisha kuvunjika kwa mechi dhidi yao na Ivory Coast.
Mawe, chupa na silaha nyingine zilirushwa na mashabiki uwanjani kabla ya Polisi kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizo mjini Dakar.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kwamba Ivory Coast imepewa ushindi wa mabao 2-0 na itafuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-2.
Nyota Manchester City, Yaya Toure akiongozwa na ulinzi wa POlisi wa kutuliza ghasia uwanjani wakati wa vurugu hizo
Mechi hiyo ilivunjika dakika ya 78, huku Ivory Coast ikiwa inaongoza mabao 2-0, shukrani kwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, aliyefunga mabao hayo yaliyosababisha vurugu.
Kutolewa huko kwa Senegal, kunawakosesha nyota wawili wa Newcastle, washambuliaji Demba Ba na Papiss Cisse fursa ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Afrika Kusini Januari mwakani.
Lakini pia upande wa pili, kufuzu kwa Ivory Coast, ni pigo kwa mabingwa wa Ligi Kuu, Man City ambayo itawakosa Yaya na Kolo Toure, wakati Arsenal itamkosa Gervinho na Newcastle Cheick Tiote.
vurugu
Kolo Toure akiwa amezibwa na Polisi