Tangu msimu uliopita, Yanga imekuwa ikigoma kuvaa jezi za
wadhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Vodacom yenye rangi nyekundu. Msimu
uliopita walibadilishiwa wakapewa jezi zenye nembo nyeusi na msimu huu pia
wamegoma hadi sasa kuvaa jezi hizo kwa sababu ya doa jekundu. Lakini leo BIN
ZUBEIRY alipotembelea mazoezi ya kikosi chao cha vijana chini ya umri
wa miaka 20, maarufu kama Yanga B, alikuta baadhi ya wachezaji wamevaa jezi
zenye kidoa chekundu, wakifanya mazoezi chini ya kocha wao, Salvatory Edward
kwenye Uwanja wa Kaunda, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar
es Salaam. Je, kidoa chekundu cha Vodacom ni haramu kwa Yanga A tu, lakini
Yanga B ruksa?
 |
Wachezaji wa Yanga B wakifanya mazoezi Uwanja wa leo. Unaweza jezi zenye nembo nyekundu ya Vodacom |
 |
Wachezaji wa Yanga B wakifanya mazoezi Uwanja wa leo mbele ya kocha wao, Salvatory Edward kulia. Unaweza jezi zenye nembo nyekundu ya Vodacom
|
|