MANCINI SASA ASEMA SERGIO BUSQUETS CHSGUO NAMBA MOJA JINA KUBWA KUTUA MAN CITY JANUARI 

Roberto Mancini amemtambulisha kiungo wa Barcelona, Sergio Busquets, mwenye umri wa miaka 24, kama mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa ambaye Manchester City watamsajili aungane na mchezaji mwenzake wa zamani, Yaya Toure.
Barcelona's Sergio Busquets
Busquets ametwaa taji nla Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona pamoja na mataji matatu ya La Liga.
Neymar anayetakiwa na Chelsea Chelsea, mwenye umri wa miaka 20, ameiweka mkao wa kula klabu hiyo ya Ligi Kuu England, baada ya kusema anataka kujifunza Kiingereza.
Kiungo wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, anatakiwa na AC Milan na klabu hiyo ya Italia iko tayari kukata dau la pauni Milioni 12 kumhamishia winga huyo Uwanja wa San Siro mwakani.
Brendan Rodgers hatatoa pauni Milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa Chelsea, Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 23, lakini kocha huyo wa Liverpool atakuwa tayari kumchukua mchezaji huyo iwapo atapewa kwa mkopo kwanza amtazame.
Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Marseille, Loic Remy, mwenye umri wa miaka 25, ifikapo January kama mbadala wa Sturridge.

TORRES AELEZEA CHELSEA ILIVYOKATA TAMAA MSIMU ULIOPITA

Fernando Torres, mwenye umri wa miaka 28, ameelezea namna Chelsea ilipofikia pabaya msimu uliopita, kwa kusema ilifikia yeye na wachezaji wenzake wakawa hawajali kama klabu itashinda au kupoteza mechi.
Arsenal's Jack Wilshere
Wilshere, mwenye umri wa miaka 20, hajaanza kwenye mechi ha ushindani tangu Juni 2011 kutokana na kuwa majeruhi.
Kiungo wa Queens Park Rangers, Joey Barton, mwenye umri wa miaka 30, ambaye anatumikia adhabu ya kukosa mechi 12, alipigwa picha mbaya akiwa na mchezaji wa Istre, Guy-Roland Niangbo katika mechi ya kirafiki na Marseille, ambako anacheza kwa mkopo.
Arsenal imeandaa mechi ya kirafiki ambayo mashabiki hawataruhusiwa kuingia katika Uwanja wao wa mazoezi wa London Colney dhidi ya Chelsea kwa ajili ya kumtazama mchezaji wake mwenye umri wa miaka 20, Jack Wilshere namna anavyorejea kwenye kikosi chake cha kwanza.

MECHI YA ENGLAND, POLAND YAAHIRISHWA

Baada ya mechi ya jana ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Poland kuahirishwa, hali ya hewa bado inaiweka matatani mechi hiyo ambayo ambayo imepangwa sasa kuchezwa leo..