Haruna Niyonzima (kulia) akiongea na Godfrey Taita wakati wa mazoezi CCM Kirumba
Kuwasili kwa wachezaji hao watatu ambao walikwenda kuzitumikia timu zao za Taifa katika michezo ya kirafiki iliyofanyika katikati ya wiki, kutakifanya kikosi cha Young Africans kukamilika wachezaji wote kufuatia wachezaji waliokuwa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kuanza mazoezi jana.
Young Africans itakua na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumatano dhidi ya timu inayoshika mkia ya African Lyon mchezo ambao utakua mzuri kwani African Lyon watataka kupata ushindi ili waweze sogea katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo huku Yanga nayo ikihitaji point 3 ili iweze kuendelea kukaa kileleni.
Kocha Mkuu Ernest Brandts mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama ametoa mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji hivyo kesho jumamosi na keshokutwa jumapili hakutakua na mazoezi na timu itaingia kambini siku ya jumapili jioni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
Aidha Brandts amesema watahakikisha wanacheza vizuri na kuibuka na ushindi katika mchezo wa jumatano ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom hatua itakayopelekea pia kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa.
Katika kikosi kilichoendelea na mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa mabatini hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja na wachezaji wote wako fit tayari kabisa kwa mpambano huo dhidi ya African Lyon