KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameilalamikia Ligi Kuu England kwa kumpangia kucheza na Everton leo, ikiwa ni siku tatu kabla ya kukutana na Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika siku ambayo Ferguson alipigwa faini ya pauni 12,000 na FA kwa kauli mbaya, pia alimropokea kocha wa kikosi cha vijana chini ya miaka 21 cha England, Stuart Pearce kwa kusema beki wa United, Phil Jones anaumwa shingles (ugonjwa fulani wa ngozi wenye kusababisha uvimbe kweney sehemu ya mwili).
Na Ferguson wazi hakuwa mwenye furaha alipoishambulia Ligi Kuu na Sky TV kwa kuwapa Madrid nafasi kuelekea mchezo wa kwanza dhidi yao Jumatano.
Sir Alex Ferguson hafurahii na mechi na Everton
Ilikuwa 4-4: Bao la Steven Pienaar dhidi ya Manchester United msimu uliopita lilimuumiza Ferguson
Manchester United itakutana na Cristiano Ronaldo na wenzake wa Real Jumatano mjini Madrid