KLABU ya Arsenal imekatwa maini na Everton usiku huu kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika kwenye Uwanja wa Emirates.
The Gunners waliingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi nne za ligi na kuzipiku Tottenham na Chelsea katika mbio za kuwania tiketi ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Pamoja na hayo, vijana wa Arsene Wenger usiku huu walishindwa kufurukuta mbele ya kikosi cha Everton side.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs/Monreal dk90, Arteta, Ramsey, Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk68, Cazorla, Walcott/Podolski dk69 na Giroud.
Everton: Howard, Baines, Gibson, Jagielka, Mirallas/Oviedo dk90, Distin, Barkley/Jelavic dk76, Pienaar, Coleman, Fellaini na Anichebe/Naismith dk90.
Hakuna njia ya kwenda popote: Licha ya jitihada nyingi, hakukuwa na bao leo
Kasheshe: Kulitokea ugomvi kati ya Jack Wilshere na Kevin Mirallas ambao uliendelea hadi mapumziko