![]() |
Wanakuja kesho; AS FAR Rabat |
Na Prince Akbar
WAPINZANI wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, msafara wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa
Azam FC ilifanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuifunga jumla ya mabao 2-1 Barack Young Contollers II ya Liberia.
Ilianza kwa kushinda 2-1 mjini Monrovia kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.