IMEWEKWA JULAI 5, 2013 SAA 12:38 ASUBUHI
KLABU ya Chelsea imekuna kichwa na kuamua kuongeza dau ili kupigania saini ya Edinson Cavani dhidi ya Paris St Germain na sasa iko tayari kutoa Pauni Milioni 50 kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Napoli.
BIN ZUBEIRY inafahamu kocha wa PSG, Laurent Blanc ametoa ofa ya Pauni Milioni 49.3 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
Chelsea na Man City sasa zitatakiwa kuvunja rekodi ya dau la usajili Uingereza, ambalo ni Pauni Milioni 50 alizotoa bilionea mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuilipa Liverpool kumnunua Fernando Torres, kama wanataka kumsaini mshambuliaji huyo gumzo kwa sasa duniani.
Anatakiwa: PSG inataka kumsaini Edinson Cavani ahamie Ufaransa msimu ujao
Cavani anatakiwa na klabu zote, lakini dau la PSG linamaanisha watatakiwa kupambana kuongeza dau kumpata mpachika mabao huyo.
Cavani alifunga dhidi ya Chelsea mwaka 2012 na wanatumai kumpata 2013
Mtu wa Pauni Milioni 50: Mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres ndiye kwa sasa anashikilia rekodi ya kusajiliwa bei chafu Uingereza
Mifuko mizito: Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich atalazimika kutonoa mifuko yake kuipata saini ya Cavani