IMEWEKWA JULAI 5, 2013 SAA 12:49 ASUBUHI
KLABU ya West Brom imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Nicolas Anelka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye kwa sasa ni huru, amesaini Mkataba mfupi wa mwaka mmoja kufanya kazi The Hawthorns.
Klabu hiyo imethibitisha kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Albion usiku huu (jana) imekamilisha usajili wa Anelka rasmi kwa mwaka mmoja,"
Dili limekamilika: Youssouf Mulumbu ameposti hii picha ya Nicolas Anelka akiwa ameshika jezi ya West Brom jana
Kocha wa Baggies, Steve Clarke, ambaye alifanya kazi na Anelka kwa muda mfupi Chelsea, amefurahishwa na usajili huo.
Mtu wa safari: Anelka amechezea Chelsea, Bolton, Liverpool, Manchester City na Arsenal zote za England
Alipokuwa kinda: Anelka aliibuka katika Ligi Kuu ya England mwaka 1997 akianzia Arsenal na akauzwa miaka miwili baadaye