IMEWEKWA JULAI 5, 2013 SAA 1:05 ASUBUHI
GARI kama la mshambuliaji Leeds United ya England na wa zamani wa Liverpool, Bolton na Blackburn, El Hadji Diouf, limelitwa sokoni, lakini kupata mnunuzi imekuwa ngumu.
Gari aina ya Cadallac Escalade la mwaka 2007, lina vikorombwezo vya zaida kama siti nyeupe za ngozi, muziki mkali na vioo vya TV.
Gari aina ya Cadillac Escalade analomiliki El Hadji Diouf
El Hadji Diouf anapenda wakati wote kuteka hisia za watu
Unataka kumiliki gari kama la Diouf?
Gari hilo limewekwa mnadani kwa kadi namba 0206 kwa punguzo la bei hadi Pauni 28,000, lakini halijamvutia yeyote hadi sasa.
"Hili ni gari kali, picha zinajieleza zenyewe, linamilikiwa na mwanasoka El Hadji Diouf, lina vikorombwezo kibao, lina mfumo mzuri wa muziki na TV na vinginevyo, lina mvuto nje na ndani,"limesema tangazo la mauzo yake.
Mwonekano wa ndani
Zuri: lina siti nyeupe za ngozi
Diouf pia anamiliki Cadillac Escalade la rangi ya dhahabu
...Na Mercedes (hilo juu) na Ranger Rover nyeupe (chini)