Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 2:56 ASUBUHI
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera amesema kwamba kipigo cha nyumbani jana kutoka wageni Uganda 1-0 katika mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini kimemuuma.
“Nimeumia. Tumeumia. Kufungwa nyumbani, hii si sawa. Ila ndiyo mpira, haikuwa bahati yetu,”alisema Bendera baada ya mechi wakati anaondoka uwanjani, kufuatia Taifa Stars kulala 1-0 jana mbele ya The Cranes.
Alipoulizwa sababu za kiufundi za Stars kufungwa jana, kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars, alisema; “Hapana, huko siwezi kuzungumzia, tumefungwa tu, imetuuma, basi,”alisema.
Kwa upande wake, Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema mpira wa miguu ni mchezo wa kufunga mabao ambapo timu ilipata nafasi nzuri katika dakika ya kwanza tu, lakini ilishindwa kuibadili kuwa bao.
“Uganda walitengeneza nafasi moja tu katika kipindi cha kwanza wakati sisi tulikuwa nazo kadhaa. Kipindi cha pili tuliwapa nafasi wakafunga bao lao. Lakini kwa kifupi kama wao wameweza kufunga hapa (Dar es Salaam), hata sisi tunaweza kufunga Kampala,” amesema Kim akizungumzia nafasi ya timu yake kusonga mbele.
Kwa upande wake, kocha wa Uganda, Milutin Sredojevich ‘Micho’ alisema kwamba alitumia udhaifu wa beki Erasto Nyoni kutengeneza mashambulizi katika mchezo wa jana.
“Ndiyo maana alipoingia Luhende (David) nikabadilisha mfumo na kucheza 4-2-3-1,”alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga SC.
Timu hizo zitarudiana jijini Kampala kati ya Julai 26 na 27 mwaka huu ambapo mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kwenda kwenye fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini. Stars ilicheza fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

![]() |
Kikosi cha Stars kilichofungwa 1-0 na Uganda jana |