IMEWEKWA JULAI 6, 2013 SAA 1:14 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI wa Wigan, Arouna Kone amekwenda kufanyiwa vipimo vya afya Everton leo huku The Toffees wakijiandaa kuipiga bao Newcastle kumnunua mchezaji huyo anayeuzwa Pauni Milioni 5.
Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez anatarajia kuungana tena na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alimfundisha akiwa Uwanja wa DW.
Mwanasoka huyo wa Ivory Coast amefunga mabao 11 katika Ligi Kuu ya England katika msimu wake wa kwanza England na aliiwezesha Wigan kutwaa Kombe la FA, lakini hajafanya siri juu ya kutaka kwake kuondoka katika klabu hiyo baada ya kushuka Mei.
Anakwenda Everton: Arouna Kone yuko karibuni kutua Goodison Park
Kone alikataa kuhamia Tyneside mapema wiki hii kwa Pauni Milioni 6.
Klabu zote zimepewa ruhusa kuzungumza na Kone aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu na Wigan msimu uliopita.