IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 4:14 USIKU
WAZI Wayne Rooney anaonekana anataka kuondoka Manchester United kabla ya mwanzo wa msimu mpya baada ya kukerwa na jinsi anavyochukuliwa juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo.
Chelsea na Arsenal zote zinamtaka mshambuliaji huyo England, ambaye ameripotiwa kukasirika na kuchanganyikiwa na jinsi anavyofanyiwa na maneno ya kocha mpya wa United, David Moyes.
Moyes amesema Rooney ni muhimu kikosini - iwapo Robin van Persie anakuwa majeruhi.
Amepasuka: Wayne Rooney ameripotiwa kukasirika na kuchanganyikiwa juu ya mustakabali wake Manchester United
Pozi la mshambuliaji: Rooney anafikiri hana zaidi cha kuthibitisha baada ya mismu tisa Old Trafford
Licha ya Van Persie kuongoza kwa ufungaji wa mabao United msimu uliopita, Rooney hafikiri tena kama anaweza kucheza nafasi ya pili kwa mtu yeyote Old Trafford.
Kwa mujibu wa Sky Sports, anafikiri hana tena cha kuthibitisha United baada ya misimu tisa, kulingana na taarifa za vyombo vya habari na ujumbe wa United.
Rooney alidumu kwa saa 24 tu katika ziara ya United kujiandaa na msimu, akarudi nyumbani baada ya kuumia nyama za paja kwa ajili ya matibabu.
Maneno hayo yaliyomkera yalichapishwa kwenye gazeti la Jumapili wakati Moyes alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Bangkok wiki iliyopita.
Jibwa kuu? Rooney anafikiri hawezi kucheza tena nafasi ya pili kwa mtu yeyote Old Trafford, hata Robin van Persie
Hakuna karibu: Habari hizi zitamshitua kocha mpya wa United, David Moyes, ambaye alimkochi Rooney Everton
Moyes alisema: "Kwa ujumla, fikra zangu kwa Wayne ni kwamba ikiwa kwa sababu yeyote Robin van Persie anaumia, tutamhitaji yeye sana,".
Hii imechukuliwa kwamba Moyes anamshusha Rooney mbele ya Mholanzi huyo mkali wa mabao.
Na akiwa ameweka nyumbani Medali za mataji manne ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa kwa jina lake, Rooney haamini kama ana chochote cha zaida cha kuthibitisha United.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alizungumzia nia yake kwa Rooney, akisema: "Ni mchezaji ninayempenda sana, lakini siwezi kusema zaidi. Ana kasi na anayepasua na ninampenda. Lakini ni mchezaji wa Manchester United player,".
Jumajne alikuwa radhi kumzungumzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipoiambia BBC Sport: "Ikiwa Wayne ni chaguo la pili kwa Man United, kisha timu ya taifa itaathirika,".
"Hiki ni kipindi ambacho klabu kubwa na makocha wao wanahusishwa na kila kitu,"alisema Mourinho. "Hadi Agosti 31, huo ndiyo utakuwa mwisho wa tetesi na ukweli utabainika,".
Akiwa anatakiwa na klabu za Chelsea na Arsenal pamoja na PSG, tayari United imetoa msimamo wake, ikisema haitamuuza mchezzji huyo kwa klabu yoyote pinzani kwao.