
IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 4:32 USIKU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Mussa Katabaro akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni ya leo tayari kwa safari ya London, Uingereza kwenda kushiriki Mkutano wa G-20 wa Ushirika wa Uwekezaji kwenye Miundombinu Afrika, unaotarajiwa kufanyika kati ya Julai 17 na 19 kwenye ukumbi wa Grosvenor Square, kwenye hoteli ya Millennium, Mayfair, London.
Katabaro ni kati ya Watanzania wawili walioalikwa kwenye Mkutano huo, utakaoshirikisha wafanya biashara wengine wakubwa duniani zaidi ya 300. Kushoto ni mwanawe, Mervine aliyemsindikiza baba yake.