IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 3:22 ASUBUHI
KLABU ya Barcelona imeifumua mabao 8-0 Santos kwenye Uwanja wa Nou Camp na kutwaa taji la Joan Gamper katika mfululizo wa maandalizi yao ya msimu.
Mchezaji aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 48.6 majira haya ya joto, Neymar alianzia benchi dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani, sambamba na nyota anayetakiwa na Manchester United, Cesc Fabregas, ingawa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal alifunga mabao mawili alipoingia kipindi cha pili.
Alexis Sanchez, Pedro na Lionel Messi kila mmoja alifunga bao moja kipindi cha kwanza, wakati bao la kujifunga la Leo, na mabao ya Adriano na Jean Marie Dongou, na mawili ya Fabregas yalihitimisha karamu hiyo ya mabao.
Mabao ya mwisho? Nyota anayetakiwa na Manchester United, Cesc Fabregas alianzia benchi lakini akafunga mabao mawili kipindi cha pili
Nyota wawili: Lionel Messi na Neymar wakifurahia kabla ya mechi
Messi (kushoto), Pedro (katikati) na Sanchez (kulia) waling'ara
La kwanza kati ya mengi? Barca imetwaa taji la Joan Gampar
Kasheshe: Neymar akilindwa dhidi ya shabiki mwenye hasira wa Internacional mjini Barcelona
Kocha mpya, Tata Martino (kulia) akimpa maelekezo Neymar


.png)