IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 3:43 ASUBUHI
KOCHA wa Barcelona, Tata Martino amepeleka pigo lingine Manchester United kuwakatisha tamaa kabisa ya kumnasa Cesc Fabregas.
United imetoa ofa ya Pauni Milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyefunga mabao mawili jana Barca ikishinda 8-0 dhidi ya Santos katika michuano ya Gamper Ijumaa usiku.
Kujiamini: Martino anaamini Fabregas, aliyecheza wakati Barca inashinda 8-0 dhidi ya Santos, atabaki Nou Camp
Mipango: Martino amesema baada ya mechi na Santos kwamba angependa Cesc abaki Barcelona
Pamoja na hayo, baada ya mechi Martino alisema: "Ningependa kwamba Cesc abaki nasi. Hakika, nitakuwa mwenye raha kusema atabaki,".
Alexis Sanchez, Pedro na Lionel Messi walifunga bao moja kila mmoja kipindi cha kwanza upande wa Barcelona Uwanja wa Nou Camp, wakati bao la kujifunga la Leo, na mabao ya Adriano na Jean Marie Dongou, pamoja na mawili ya Fabregas yalihitimisha ushindi wa 8-0.
United inacheza na mechi ya kirafiki na Real Betis katika Uwanja ambao mashabiki hawataingia leo lakini chini ya David Moyes hawajasajili mchezajli mchezaji mpya.
Mawili nyavuni: Fabregas ameifungia mabao mawili jana Barca


.png)