• HABARI MPYA

    Saturday, August 03, 2013

    AZAM HAOOO, WAPAAA SAUZI KWENDA KUKUSANYA NGUVU ZA KUSHIKISHA ADABU YANGA

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 7:19 MCHANA
    AZAM FC imeondoka mchana huu kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini, kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya.
    Timu hiyo yenye maskani yake, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, imeondoka na kikosi chake kizima, kasoro wachezaji wawili tu majeruhi, kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony.
    Kwa Madiba; Kutoka kulia kocha Msaidizi, Kali Ongala, Kocha Mkuu, Stewart Hall na wachezaji Himid Mao na Aggrey Morris wakiwa Uwanja wa ndege tayari kwa safari ya Afrika Kusini 

    Akizungumza wakati timu hiyo inaelekea kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari, Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall alisema wanatarajia kambi hiyo itakuwa na manufaa.

    RATIBA YA MECHI ZA AZAM AFRIKA KUSINI...

    AGOSTI 5, 2013;   Kaizer Chiefs
    AGOSTI 7, 2013;   Mamelodi Sundowns 
    AGOSTI 9, 2013;   Orlando Pirates
    AGOSTI 12, 2013; Moroka Swallows.
    “Tumepata mazingira mazuri ya kambi, Uwanja wa mazoezi na mechi nzuri za kujipima nguvu. Vijana watanufaika sana na kambi hii na itakuwa sababu ya kufanya vizuri katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, tukianza na kuchukua Ngao,”alisema.
    Ikiwa nchini humo, Azam itacheza mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya Kaizer Chiefs Agosti 5, Mamelodi Sundowns Agosti 7, Orlando Pirates Agosti 9 na Agosti 12 dhidi ya Moroka Swallows.
    Kuna uwezekano Azam ikacheza mechi zaidi kulingana na namna ambavyo timu zaidi nchini humo zitavuwiwa kucheza nayo.
    Kutoka kulia Waziri Salum, John Bocco na Aishi Manula

    Azam inatarajiwa kurejea nchini siku moja kabla ya kucheza mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Safari hii Azam, washindi wa pili mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu wamepania kutwaa Ngao mbele ya Yanga, baada ya mwaka jana kufungwa na Simba SC na kocha Muingereza Stewart Hall anajiandaa kikamilifu kwa ajili hiyo.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM HAOOO, WAPAAA SAUZI KWENDA KUKUSANYA NGUVU ZA KUSHIKISHA ADABU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top