• HABARI MPYA

    Thursday, August 08, 2013

    LIVERPOOL YAONYESHA INAWEZA MAISHA BILA SUAREZ...YAPIGA MTU NNE LEO

    IMEWEKWA AGOSTI 7, 2013 SAA 5:50 USIKU
    LIVERPOOL imeonyesha inaweza kuishi bila Luis Suarez anayetaka kuondoka, baada ya kuendelea vema na mechi zake za kujiandaa na msimu.
    Pamoja na habari za Luis Suarez kuondoka kuwa ajenda kuu kwa sasa, kikosi cha Brendan Rodgers leo kimeifumua valeranga mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Ullevaal, mjini Oslo, Norway katika mchezo wa kirafiki.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao ya leo, Luis Alberto, Iago Aspas, Martin Kelly na Raheem Sterling katika mchezo wa leo, Liverpool ikishuhudiwa na mmiliki wake, John W Henry kwa mara ya kwanza baada ya miezi 13 ikiweka rekodi ya kushinda mechi ya sita.
    Alberto alifunga dakika ya 31, Aspas dakika ya 42, Kelly dakika ya 54 na Sterling dakika ya 90, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Giancarlo Gonzalez dakika ya 35.
    Kikosi cha Liverpool leo kilikuwa: Jones/Mignolet dk46, Alberto/Coutinho dk46, Aspas/Borini dk46, Henderson/Gerrard dk46, Coates/Toure dk46, Downing/Sterling dk46, Spearing/Kelly dk46, Allen/Lucas dk46, Flanagan/Enrique dk46, Ibe/Assaidi dk46 na Wisdom.
    Valerenga: Kongshavn/Knutsen dk85, Larsen/Wawrzynkiewicz dk51, Gonzalez, Hogh, Lecjaks, Ogude/Nasberg dk62, Zajic/Haested dk57, Holm/Zahid dk57, Fellah, Berre/Borven dk67 na Calvo.
    Victory: Liverpool beat Valerenga 3-1 in a pre-season friendly at Olso's Ullevaal Stadium
    Ushindi: Liverpool imeifunga Valerenga 3-1 kwenye Uwanja wa Ullevaal, Oslo leo
    Breakthrough: Joe Allen watches Luis Alberto's (not pictured) shot find the bottom corner
    Joe Allen akishuhudia shuti la Luis Alberto (hayupo pichani) likitinga nyavuni
    Slotted: Iago Aspas put Liverpool back ahead from close range just before half-time
    Iago Aspas akiifungia Liverpool kabla ya mapumziko
    Popular: Liverpool fans in Oslo show their support for Brendan Rodgers' team
    Mashabiki wa Liverpool mjini Oslo wakionyesha kumuunga mkono kocha Brendan Rodgers na timu yake
    Under pressure: Joe Allen plays a pass as Valerenga's Mohamed Fellah closes in
    Joe Allen akitoa pasi huku akizongwa na mchezaji wa Valerenga, Mohamed Fellah
    On the mic: Liverpool legend Ian Rush is interviewed on the field at half-time
    Kwenye kipaza: Gwiji wa Liverpool, Ian Rush akifanyiwa mahojiano wakati wa mapumziko
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIVERPOOL YAONYESHA INAWEZA MAISHA BILA SUAREZ...YAPIGA MTU NNE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top