Na Mahmoud Zubeiry, Johannesburg, Afrika Kusini, IMEWEKWA AGOSTII 8, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
KABLA ya Azam kwenda kumenyana na Mamelodi Sundown jana, nilitoka pamoja na Kocha Mkuu wa klabu, Muingereza Stewart Hall, Msaidizi wake, Kali Ongala na Meneja, Jemadari Said kwenda kununua vifaa vya timu kama maji na kadhalika eneo la Randburg.
Tukiwa njiani, Stewart alianza kunipa habari kuhusu Mamelodi kwamba ni klabu tajiri, iliyowekeza vizuri na hata safari ya kwenda Chloorkop, kutoka Randburg ilipoanza nilikuwa na shauku kubwa ya kujua zaidi kuhusu Mamelodi.
Tulipofika, kabla sijaambiwa chochote nilijua tu hapa ndipo maskani ya klabu ya Mamelodi- rangi za kijani na njano zilizopamba uzio wa makao makuu ya klabu hiyo na maandishi na nembo ya klabu yalitosha kunifanya nijue ni pale tunapokwenda.
Tulipoingia ndani, nilipotazama Uwanja wa Mamelodi, kwanza nikajiridhisha haufikii ubora wa Uwanja wa Azam FC pale Chamazi, Dar es Salaam- sana vitu vidogo vidogo ni zaidi kama ofisi na mpangilio wa vitu, lakini Azam Complex ni bora zaidi.
Sikuona gym ya kisasa kama ile ya Chamazi ama bwawa la kuogelea au majukwaa- lakini yote kwa yote, Mamelodi wana maskani bora ambayo wanaendelea kuiboresha.
Mara moja nikamdaka Ofisa Habari wa klabu, Kabelo Mosito na kuanza kumuuliza masuala mbalimbali kuhusu klabu hiyo na akanipa ushirikiano mkubwa- kiasi cha hadi kunitembeza na kunielekeza kila kitu kuhusu klabu yao.
Wana viwanja vinne ndani ya maskani yao, vinavyotumika kwa timu tofauti, ukiachilia mbali ile ya wakubwa ya Ligi Kuu iliyofungwa 1-0 na Azam jana, kuna za vijana pia.
Wana ofisi nzuri, Maktaba nzuri ya kutunzia kumbukumbu mbalimbali na muhimu za klabu, ikiwemo picha za magwiji wao, vikosi vya misimu iliyopita na mataji.
Niseme nini kuhusu Mamelodi- zaidi ya kuzisikitikia klabu zetu kongwe Tanzania, Simba na Yanga kwamba zimekosa viongozi wabunifu na wenye nia ya dhati ya kuzitafutia maendeleo klabu hizo.
Wazi Simba na Yanga zina wasimamizi tu kuhakikisha timu zinasajili, zinashiriki Ligi Kuu tu basi, lakini suala la viongozi hakika ni sifuri.
Ukirejea miaka ya nyuma, waasisi wa klabu wameacha kumbukumbu ya majengo ambayo yanatumika sasa na kwa Yanga SC hadi Uwanja wa Kaunda, ambao viongozi wake wa sasa wameutelekeza na kuzidi kuharibika.
Kitu kimoja ni kwamba, Simba na Yanga ni timu ambazo zina wapenzi kila kona ya nchi- leo hii hata zikihamishia maskani zake Kisarawe, kabla ya kufikiria watu watazifuata, lakini kuke kule zina wapenzi kibao.
Lakini imeshindikana kabisa klabu hizo kufikiria kuwa na viwanja vyake hata nje ya mji. Simba SC watasema watajenga wapi Uwanja pale Msimbazi- na Yanga SC watasingizia mafuriko wanahofia kuingia hasara. Sawa.
Lakini vipi kuhusu kununua maeneo nje ya mji na kuwekeza mradi mfano wa Mamelodi iliyofanya Chloorkop, kwa kuwa labda kufanya kama Azam ni gharama zaidi.
Uzio wa kuuzunguka Uwanja- kuotesha nyasi na kutengeneza viwanja japo vitatu vya mazoezi kwa ajili labda ya timu za vijana na wakubwa. Kujenga bweni la wachezaji, ofisi na vitu vingine vidogo vidogo inawezekana wakipatikana viongozi kweli.
Katika hili, Simba na Yanga SC hazihitaji fedha kutoka mfukoni mwa yeyote- wengi wetu tunajua gharama za viwanja nje ya mji na tunajua gharama za ujenzi, suala hilo lipo ndani ya uwezo wa klabu hizo kutokana na mapato ya mechi zake tu, iwapo zitaweka utaratibu mzuri na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Lakini Simba na Yanga baada ya kusajili wachezaji kwa mamilioni mengi, kuwapangia mishahara mizuri, bado ili washinde wanawashawishi kwa ahadi za fedha ambazo mara nyingi hutokana na mapato ya mechi. Lini klabu itatumia fedha hizo kwa maendeleo yake ya msingi?
Zimeshindwa kutumia nembo zao kujinufaisha kibiashara licha ya kuwa na mamilioni ya mashabiki nchi nzima. Simba na Yanga SC kama zinakuwa na viongozi wa kweli, zinaweza kuvutia makampuni mengi kuingia nao mikataba.
Azam FC wanapasua mawimbi na miaka 10 ijayo watakuwa kitu kikubwa Afrika iwapo wataendelea hivi- wakati Simba na Yanga SC zinazidi kudidimia kwa sababu zimekosa viongozi, zina wasimamizi tu.
Fedha zilizotumika kwa ziara ya Yanga SC Uturuki Desemba mwaka jana- sijui kama zingetumika kwa mradi wa ujenzi wa maskani mpya ya klabu ingekuwa faida kiasi gani kwao.
Lakini kwa kuwa walichagua ufahari- wanaendelea kunyanyaswa pale sekondari ya Loyola, Mabibo- wakikatishwa programu zao za mazoezi kupisha sherehe za wanafunzi. Fedheha iliyoje! Hapo hapo, eti wanataka wapewe mgawo zaidi wa haki za Televisheni Ligi Kuu, kwa lipi?
Umefika wakati sasa mashabiki wa Simba SC na Yanga SC wabadilike na wawape wakati mgumu viongozi wao juu ya maendeleo ya klabu zao- maana haiyumkiniki hadi leo klabu hizo hazina japo viwanja vya mazoezi na wanachama wameendelea kudanganywa kila siku.
Simba na Yanga SC wana mengi ya kujifunza kutoka Mamelodi ambayo tangu mwaka 2003, inamilikiwa na bilionea mfanyabishara wa madini, Patrice Motsepe ikifahamika kwa jina la utani kama The Brazilians ‘Wabrazil’ kutokana na kuvaa jezi za kijani na njano kama timu ya taifa ya Brazil.
Kihistoria haina tofauti sana na vigogo hao wa soka Tanzania, kwani ilianzishwa mwanzoni mwa miaka 1960 na kikundi cha vijana wadogo, miongoni mwao wakiwemo Reginald Hartze, Joey Lawrence na Bernard Hartze.
Lakini Simba na Yanga zinaweza kuwa kama Mamelodi leo, iwapo tu zitapata viongozi watakaojitoa kwa maendeleo ya klabu hizo na si wasimamizi kama ilivyo sasa. Eid Mubarak.
KABLA ya Azam kwenda kumenyana na Mamelodi Sundown jana, nilitoka pamoja na Kocha Mkuu wa klabu, Muingereza Stewart Hall, Msaidizi wake, Kali Ongala na Meneja, Jemadari Said kwenda kununua vifaa vya timu kama maji na kadhalika eneo la Randburg.
Tukiwa njiani, Stewart alianza kunipa habari kuhusu Mamelodi kwamba ni klabu tajiri, iliyowekeza vizuri na hata safari ya kwenda Chloorkop, kutoka Randburg ilipoanza nilikuwa na shauku kubwa ya kujua zaidi kuhusu Mamelodi.
![]() |
Lango Kuu; Mwonekano wa nje wa ya lango kuu la kuingia makao makuu ya Mamelodi |
Tulipofika, kabla sijaambiwa chochote nilijua tu hapa ndipo maskani ya klabu ya Mamelodi- rangi za kijani na njano zilizopamba uzio wa makao makuu ya klabu hiyo na maandishi na nembo ya klabu yalitosha kunifanya nijue ni pale tunapokwenda.
Tulipoingia ndani, nilipotazama Uwanja wa Mamelodi, kwanza nikajiridhisha haufikii ubora wa Uwanja wa Azam FC pale Chamazi, Dar es Salaam- sana vitu vidogo vidogo ni zaidi kama ofisi na mpangilio wa vitu, lakini Azam Complex ni bora zaidi.
![]() |
Hapa ni mbele la mlango wa kuingia ofisi kuu, nikiwa na Kocha wa U20 ya Mamelodi, Noel Mzala |
![]() |
Nipo mbele ya kabati la mataji ya klabu. |
![]() |
Naacha kumbukumbu zangu katika jezi ambayo wageni maalum husaini wanapofika hapo
|
Mara moja nikamdaka Ofisa Habari wa klabu, Kabelo Mosito na kuanza kumuuliza masuala mbalimbali kuhusu klabu hiyo na akanipa ushirikiano mkubwa- kiasi cha hadi kunitembeza na kunielekeza kila kitu kuhusu klabu yao.
Wana viwanja vinne ndani ya maskani yao, vinavyotumika kwa timu tofauti, ukiachilia mbali ile ya wakubwa ya Ligi Kuu iliyofungwa 1-0 na Azam jana, kuna za vijana pia.
Wana ofisi nzuri, Maktaba nzuri ya kutunzia kumbukumbu mbalimbali na muhimu za klabu, ikiwemo picha za magwiji wao, vikosi vya misimu iliyopita na mataji.
![]() |
Hii ni ofisi ya Uhusiano, nikiwa na Ofisa Habari wa klabu, Kabelo Mosito. Ndugu zetu Baraga Kizuguto na Ezekiel Kamwaga vipi?
|
![]() |
Nipo na Miss Mamelodi 2012, Kerusha Kylie Govender
|
![]() |
Niko Katibu wa klabu, Joe Latakgomo
|
![]() |
Mamelodi wananifaika na nembo yao kwa kuuza jezi, kuvutia makampuni wadhamini kama sasa wanadhaminiwa na Honda na Nike
|
![]() |
Gari la Kerusha alilopewa na wadhamini wa Mamelodi, Honda. Klabu inatumia magari ya Honda tu na ua wao umechakaa magari ya aina mbalimbali.
|
Niseme nini kuhusu Mamelodi- zaidi ya kuzisikitikia klabu zetu kongwe Tanzania, Simba na Yanga kwamba zimekosa viongozi wabunifu na wenye nia ya dhati ya kuzitafutia maendeleo klabu hizo.
Wazi Simba na Yanga zina wasimamizi tu kuhakikisha timu zinasajili, zinashiriki Ligi Kuu tu basi, lakini suala la viongozi hakika ni sifuri.
Ukirejea miaka ya nyuma, waasisi wa klabu wameacha kumbukumbu ya majengo ambayo yanatumika sasa na kwa Yanga SC hadi Uwanja wa Kaunda, ambao viongozi wake wa sasa wameutelekeza na kuzidi kuharibika.
Kitu kimoja ni kwamba, Simba na Yanga ni timu ambazo zina wapenzi kila kona ya nchi- leo hii hata zikihamishia maskani zake Kisarawe, kabla ya kufikiria watu watazifuata, lakini kuke kule zina wapenzi kibao.
![]() |
Uwanja wa Mamelodi
|
![]() |
Upande wa uwanjani, ndivyo unavyoweza kuziona ofisi za Mamelodi
|
![]() |
Upande mwingine wa eneo la klabu
|
![]() |
Na huku pia. Majengo ya kushoto ndiko wachezaji huenda kubadilishia nguo kuingia mazoezini na huko ndiko kuna gym pia
|
Lakini imeshindikana kabisa klabu hizo kufikiria kuwa na viwanja vyake hata nje ya mji. Simba SC watasema watajenga wapi Uwanja pale Msimbazi- na Yanga SC watasingizia mafuriko wanahofia kuingia hasara. Sawa.
Lakini vipi kuhusu kununua maeneo nje ya mji na kuwekeza mradi mfano wa Mamelodi iliyofanya Chloorkop, kwa kuwa labda kufanya kama Azam ni gharama zaidi.
Uzio wa kuuzunguka Uwanja- kuotesha nyasi na kutengeneza viwanja japo vitatu vya mazoezi kwa ajili labda ya timu za vijana na wakubwa. Kujenga bweni la wachezaji, ofisi na vitu vingine vidogo vidogo inawezekana wakipatikana viongozi kweli.
Katika hili, Simba na Yanga SC hazihitaji fedha kutoka mfukoni mwa yeyote- wengi wetu tunajua gharama za viwanja nje ya mji na tunajua gharama za ujenzi, suala hilo lipo ndani ya uwezo wa klabu hizo kutokana na mapato ya mechi zake tu, iwapo zitaweka utaratibu mzuri na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Lakini Simba na Yanga baada ya kusajili wachezaji kwa mamilioni mengi, kuwapangia mishahara mizuri, bado ili washinde wanawashawishi kwa ahadi za fedha ambazo mara nyingi hutokana na mapato ya mechi. Lini klabu itatumia fedha hizo kwa maendeleo yake ya msingi?
Zimeshindwa kutumia nembo zao kujinufaisha kibiashara licha ya kuwa na mamilioni ya mashabiki nchi nzima. Simba na Yanga SC kama zinakuwa na viongozi wa kweli, zinaweza kuvutia makampuni mengi kuingia nao mikataba.
Azam FC wanapasua mawimbi na miaka 10 ijayo watakuwa kitu kikubwa Afrika iwapo wataendelea hivi- wakati Simba na Yanga SC zinazidi kudidimia kwa sababu zimekosa viongozi, zina wasimamizi tu.
Fedha zilizotumika kwa ziara ya Yanga SC Uturuki Desemba mwaka jana- sijui kama zingetumika kwa mradi wa ujenzi wa maskani mpya ya klabu ingekuwa faida kiasi gani kwao.
Lakini kwa kuwa walichagua ufahari- wanaendelea kunyanyaswa pale sekondari ya Loyola, Mabibo- wakikatishwa programu zao za mazoezi kupisha sherehe za wanafunzi. Fedheha iliyoje! Hapo hapo, eti wanataka wapewe mgawo zaidi wa haki za Televisheni Ligi Kuu, kwa lipi?
Umefika wakati sasa mashabiki wa Simba SC na Yanga SC wabadilike na wawape wakati mgumu viongozi wao juu ya maendeleo ya klabu zao- maana haiyumkiniki hadi leo klabu hizo hazina japo viwanja vya mazoezi na wanachama wameendelea kudanganywa kila siku.
![]() |
Nikiwa na kocha Mkuu wa Mamelodi, Pitso Masomane na wachezaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba kulia na Salum Abubakari baada ya mechi jana. Masomane alivutiwa na soka ya Azam