IMEWEKWA AGOSTI 4, 2013 SAA 1:58 ASUBUHI
UKISTAAJABU ya Mussa, utaona ya Firauni. Naama sadakta, hakika aliyeleta usemi huu hakuwa mbali na ukweli. Wiki hii Mwenyekiti wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji ameitisha Mkutano na Waandishi wa Habari, lengo kuu likiwa ni kupinga Mkataba wa haki za TV wa Ligi Kuu ya Bara.
Bodi ya Ligi Kuu imeingia Mkataba na kampuni mpya ya Habari, Azam TV kurusha mechi za Ligi Kuu na Yanga ni klabu pekee iliyopinga, Mwenyekiti wake akitoa sababu lukuki, nyingine hata haziingii akilini.
Kwa mfano suala la mauzo ya Mrisho Ngassa kutoka Azam kwenda Simba, wakati Yanga pia walikuwa wanamataka, wanadai eti Azam ina uswahiba na Simba ndiyo maana iliamua kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani wao.
Wengi tunakumbuka sakata hilo, Azam ilitangaza kumuuza mchezaji huyo na Yanga walichotarajia kuwa wangempata bure kwa sababu alikwishaonyesha ana mapenzi na klabu hiyo, hivyo mwisho wa siku angekwenda tu Jangwani.
Lakini na Ngassa naye anapenda fedha kwa sababu ndiyo maisha- Simba wakampa fedha na gari badala ya maneno matupu ya Yanga, akasaini na uongozi wa Azam ukapokea Milioni 25 ukamuidhinisha kwenda Msimbazi.
Suala la vurugu za mechi ya Yanga na Azam mwaka juzi- wachezaji wa Yanga wakati huo hawakuwa na nidhamu, walimpiga refa na walistahili adhabu. Kama Manji atataka kusema Yanga ilionewa na refa mwaka juzi ikafungwa 3-0 na Azam na zile 5-0 za Simba mwaka huo huo, ilionewa na nani?
Wakubali tu, Yanga yao wakati huo ilikuwa mbovu na ndiyo maana wachezaji wengi wa wakati huo wamekwishatupiwa virago akiwemo ‘bondia’ Stefano Mwasyika aliyemtwanga ngumi ya kitaalamu refa dhidi ya Azam siku hiyo- bila shaka wamebaki Haruna Niyonzima, Athumani Iddi ‘Chuji’ na Nadir Haroub Niyonzima pekee kutoka Yanga ya mwaka juzi.
Suala la Azam FC kucheza Ligi Kuu na wakati huo huo kununua haki za TV za Ligi Kuu, pia si hoja kwa sababu Afrika Kusini kuna Supersport United pale PSL na Supersport TV wana haki za TV za ligi hiyo. Supersort TV wana haki za TV za CAF pia wakati klabu yao hufuzu kucheza michuano ya klabu Afrika.
Kwa ujumla suala hili la haki za TV ni la uelewa na maelewano. Simba na Yanga zilipewa fungu la ziada na Azam TV kupitia programu ya vipindi maalum vya klabu zao, Simba TV na Yanga TV- yaani zaidi ya gawio la haki za TV za Ligi Kuu, kuna fedha nyingine za vipindi hivyo, tofauti na timu nyingine za ligi hiyo.
Simba wameelewa, wamesaini na watapata zaidi ya Sh. Milioni 200, ikiwa ni Milioni 100 zaidi ya klabu nyingine. Star TV waliwahi kununua haki za TV za Ligi Kuu na kila klabu ilipewa kiasi cha Milioni 5 kwa msimu na ambazo klabu nyingine hadi leo zinalalamika hazikupata.
Supersport walikuwa wanakuja kurusha michuano yetu bure na tukawa tunachekelea kama mazuzu, kisa tu mpira wetu unaonekana kwenye Luninga- sasa anakuja Azam TV na anatupa fedha bado tunaleta mizengwe.
Narejea Mkutano Mkuu wa TFF mwezi uliopita, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema maadaui wakubwa wa soka ya Tanzania ni watatu, ambao ni majungu, fitina na umbeya na katika sakata hili la Yanga na Azam TV unaweza kupata picha fulani. Fitina.
Yanga haina rekodi ya kuuza haki za TV wala kuwa na kipindi maalum cha klabu hiyo- hii inatokea kwa mara ya kwanza watu wanaleta mizengwe. Clouds TV waliwahi kuingia Mkataba wa Sh. Milioni 20 kwa mwaka na Simba SC kwa ajili ya Simba TV, kwa sababu Ruge Mutahaba ni Simba mzuri na alitumia fursa yake ya kuwa Mkurugenzi wa chombo hicho cha habari kuipa dili klabu yake, vipi Yanga?
Hili ni suala la uelewa- Azam hawaingii Mkataba wa kuidhamini Yanga. Yanga haitakuwa na mzigo wa kutangaza bidhaa yoyote ya Azam, bali kuonyesha mechi za Yanga za Ligi Kuu tu na watazirusha mechi zao pamoja na jezi zao za matangazo ya bia ya Kilimanjaro. Hawawezi kufanya kinyume. Upande wa pili, ni faida kwa mdhamini wao pia TBL.
Hoja nyingine eti Mkataba huo utazuia vyombo vya habari kuandika na kuchukua picha za Ligi Kuu- ni upotoshaji kwa sababu Ligi nyingi duniani zina mikataba ya haki za TV, lakini bado vyombo vingine vya habari vinarusha habari zake.
Sasa Yanga SC wanakataa Milioni zaidi ya 200 kwa msimu, pasipo kuwa na mzigo wa kutangaza bidhaa yoyote ya Azam FC- maana yake wanakosa wao na kwa mechi zao za ugenini za Ligi Kuu zote zitaonyeshwa na Azam TV watake wasitake- hiyo ndiyo sheria.
Ruvu Shooting Vs Yanga, Azam Vs Yanga, JKT Ruvu Vs Yanga, Ashanti Vs Yanga, Simba VS Yanga zote za Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Azam TV watarusha na baada ya hapo watakwenda Mkwakwani na Coastal, Ally Hassan Mwinyi na Rhino, Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya na City na Bukoba dhidi ya Kagera. Nini maana yake, imekula kwao Yanga.
Sote tunafahamu Yussuf Manji ni mfanyabiashara mkubwa kama Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa, hawa watu wangeweza kuketi meza moja na kumaliza hili suala bila ‘kuripuana’ kwenye vyombo vya habari. Na zadi Bakhresa ni mtu safi nchi inajua na hana tatizo na mtu yeyote, unapokorofishana naye, wewe ndiye utaonekana mkorofi kwa vyovyote.
Hili ni suala la uelewa zaidi. Linahitaji mtu kulielewa kwanza kabla ya kukurupuka kulizungumzia. Ajabu mtu hajui hata kuandika jina lake tu, anakwenda anazungumza mbele ya Waandishi wa Habari kupinga Azam TV. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni. Ramadhan Kareem waungwana inshaallah.

.png)