IMEWEKWA AGOSTI 4, 2013 SAA 11:35 ALFAJIRI
WACHEZAJI Wayne Rooney, Nani, Nemanja Vidic na Javier Hernandez wote walianza kikosini Manchester United katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Real Betis ambao mashabiki hawakuingia Uwanja wa Carrington.
Mshambuliaji wa England, Rooney alicheza kipindi cha kwanza lakini hakuweza kufunga bao, mabingwa hao wa Ligi Kuu England wakishinda 3-0.
Mchezo huo uliochezwa asubuhi ya jana kwenye Uwanja huo wa mazoezi wa United, ulikuwa wa kwanza kwa Rooney baada ya kuumia katika mechi ya kwanza ya ziara ya Mashariki ya Mbali mwezi uliopita.
Akiwasili: Rooney akiwasili kwenye Uwanja wa mazoezi wa Carrington juzi
Amerudi: Rooney alicheza dhidi ya Real Betis
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye hajatulia, amepona maumivu ya nyama za paja aliyoyapata katika ziara ya Asia ya klabu hiyo na jana alionyesha yuko sawa akicheza dhidi ya timu hiyo ya La Liga.
Rooney anatarajiwa kuhama Old Trafford kutimkia Chelsea, ambao ofa yao ya pili ya Pauni Milioni 23 ilipigwa chini.
Anaweza kuwa na mazungumzo zaidi na kocha David Moyes wiki ijayo juu ya mustakabali wake wakati United ikijiandaa kwa mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya AIK mjini Stockholm. Lakini United inabaki na msimamo wake wa kumbakiza.
Amerudi kazini: Beki Nemanja Vidic akipambana na George Ray wa Crewe Jumatatu
Milango imefungwa: Vidic alianza jana katika mchezo ambao ulichezwa milango imefungwa


.png)