IMEWEKWA AGOSTI 4, 2013 SAA 11:23 ALFAJIRI
LIVERPOOL imeshinda 2-0 dhidi ya Olympiakos ya Ugiriki katika mchezo maalum wa kumuaga Nahodha wake, Steven Gerrard baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 15.
Mabao ya Wekundu hao wa Anfield katika mchezo huo yalifungwa na Joe Allen dakika ya 23 na Henderson dakika ya 62.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet/Jones dk85 Johnson, Toure/Carragher dk62, Agger, Enrique; Allen/Henderson dk62, Gerrard/Spearing dk85, Lucas, Coutinho/Fowler dk72, Sterling/Alberto dk72 na Aspas/Suarez dk62.
Olympiacos: Megyeri, Maniatis, Fejsa, Mitroglou/Saviola dk56, Samaris/Weiss dk46, Holebas, Medjani/Manolas dk56, Slovas, Siovas, Campbell, Salino na Dominguez.
Tukio kubwa: Steven Gerrard (kulia) na Joe Allen wakishangilia baada ya bao la kwanza
La pili: Jordan Henderson alifunga la pili sekunde 12 baada ya kuingia uwanjani
Luis Suarez alicheza kwa Liverpool jana
Kipenzi cha mashabiki: Suarez akimiliki mpira upande wa mashabiki


.png)