• HABARI MPYA

    Sunday, August 04, 2013

    ARSENAL YATOKA NYUMA 2-0 NA KUPATA SARE YA 2-2 NA NAPOLI...NA INGESHINDA 3-2 KAMA REINA ASINGECHEZA PENALTI YA PODOLSKI

    IMEWEKWA AGOSTI 4, 2013 SAA 11:00 ALFAJIRI
    KLABU ya Arsenal jana ilitoka nyuma kwa mabao mawili na kupata sare ya 2-2 mbele ya timu ya kocha Rafael Benitez, Napoli katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe lao la Emirates.
    Lorenzo Insigne na Goran Pandev waliwafungia mabao wageni kipindi cha kwanza, katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu, Gunners wakionekana kuzidiwa kipindi cha kwanza.
    Hata hivyo, The Gunners walizinduka na kufanikiwa kusawazisha mabao yote, moja la Olivier Giroud kwa tika tak dakika ya 71 na lingine Laurent Koscielny kwa kichwa dakika ya 85, baada ya Insigne kufunga dakika ya saba na Pandev dakika ya 29.
    Arsenal walipata nafasi ya kufunga bao la tatu, lakini mkwaju wa penalti wa Lukas Podolski uliokolewa na kipa Pepe Reina wa Napoli.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski; Jenkinson/Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Wilshere, Gnabry/Walcott, Rosicky, Podolski na Giroud.
    Napoli: Reina; Mesto, Cannavaro, Britos, Armero, Behrami, Inler, Hamsik, Insigne, Callejon/Maggio, Pandev/Higuain.
    Respect: Arsene Wenger (right) and Rafael Benitez (left) share a word before the 2-2 draw
    Heshima: Arsene Wenger (kulia) akisalimiana na Rafael Benitez (kushoto) kabla ya mechi yao iliyoisha kwa 2-2First goal: Lorenzo Insigne celebrates Napoli's opener
    Bao la kwanza: Lorenzo Insigne akishangilia bao la kwanza aliloifungia Napoli
    Outrage: Players surround the referee after a penalty is given to Arsenal, which was subsequently saved by Pepe Reina (second left) from Lukas Podolski
    Nzugwe: Wachezaji wakiwa wamemzingira refa baada ya Arsenal kupewa penalti, ambayo iliokolewa na Pepe Reina (wa pili kushoto) baada ya Lukas Podolski kupiga.
    Uh-oh: Goran Pandev doubles the Italian side's advantage
    Uh-oh: Goran Pandev alifunga la pili kwa Napoli
    Take that: But Girouds acrobatic strike helped start a second half comeback
    Tik tak: Giroud aliifungia Arsenal kwa tik tak
    Take that: Gonzalo Higuain is tackled by Laurent Koscielny
    Chukua hiyo: Gonzalo Higuain akikabiliana na Laurent Koscielny
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YATOKA NYUMA 2-0 NA KUPATA SARE YA 2-2 NA NAPOLI...NA INGESHINDA 3-2 KAMA REINA ASINGECHEZA PENALTI YA PODOLSKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top