IMEWEKWA AGOSTI 5, 2013 SAA 4:11 USIKU
KLABU ya Tottenham imekamilisha usajili wa rekodi wa Roberto Soldado kutoka Valencia baada ya mchezaji huyo kufuzu vipimo vya afya.
Baada ya kubebwa na mabao ya Gareth Bale msimu uliopita, kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas amefanya usajili wa mchezaji kipaumbele chake majira haya ya joto na sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, Soldado anaanza kazi White Hart Lane baada ya kukamilisha usajili mchana wa leo.
Muuwaji huyo wa Hispania, ambaye amefunga mabao 30 katika mechi 46 alizoichezea Valencia msimu uliopita, ameigharimu Tottenham Pauni Milioni 26- jambo linalomfanya awe mchezaji ghali wa klabu hiyo kihistoria.
Amepewa jezi: Soldado akiwa na jezi ya Tottenham katika viwanja vya mazoezi 
Akionyesha jezi: Robert Soldado amekamilisha usajili wa Pauni Milioni 26 kutua Tottenham
Mtu mpya: Mspanyola aliyeweka rekodi ya mchezaji ghali Tottenham