IMEWEKWA AGOSTI 7, 2013 SAA 1:4 ASUBUHI
HATIMAYE Luis Suarez amevunja ukimya na kutaka aruhusiwe kuondoka Liverpool huku akiwatuhumu waajiri wake kutoheshimu ahadi waliyowekeana.
HATIMAYE Luis Suarez amevunja ukimya na kutaka aruhusiwe kuondoka Liverpool huku akiwatuhumu waajiri wake kutoheshimu ahadi waliyowekeana.
Baada ya maneno mengi, mwanasoka huyo huyo wa kimataifa wa Uruguay ameweka mambo hadharani akiiambia Liverpool anataka kuhamia klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa, kama Arsenal, timu pekee ambayo hadi sasa imetoa ofa ya kutaka kumsajili.
Suarez anajiandaa kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka mwishoni mwa wiki ili kutimiza malengo yake, huku akisema anaungwa mkono na PFA na pia anajiandaa kuifungulia mashitaka klabu hiyo kwa bodi ya Ligi Kuu ili imeuhusu kuhamia Emirates.
Mwenye mpira: Suarez ameiambia Liverpool kwamba anataka kuondoka baada ya kusema klabu imeshindwa kutimiza ahadi yake
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 angejiunga na Juventus msimu uliopita, lakini amesema alibaki kwa heshima ya Liverpool na walikubaliana ikiwa Liverpool itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa msimu wa kwanza wa Brendan Rodgers, angeruhusiwa kuondoka.
"Nilitoa kila kitu msimu uliopita, lakini haikutosha kutufanya tumalize ndani ya nne bora - sasa ninachotaka tu ni kwa Liverpool kuheshimu makubaliano,"amesema Suarez.
"Nina maneno ya klabu na tuna Mkataba wa maandishi na nitafurahi kupeleka hili suala kwa bodi ya Ligi Kuu wakaamue kesi hii, lakini sitaki ifike huko.
Ametemwa: Luis Suarez hatacheza dhidi ya Valerenga baada ya kuachwa kikosini kutokana na maumivu
"Nina miaka 26. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa. Nimesubiri mwaka mmoja na hakuna hata mmoja anayeweza kusema sikujitoa kwa kila kitu msimu uliopita ili kusaka nafasi ya kufika huko," alisema.
Suarez amesema kuna makubaliano katika Mkataba wao kwamba Liverpool lazima imuuze ikitokea klabu itakayotoa ofa ya Pauni Milioni 40, ambayo Arsenal iliitoa wiki mbili zilizopita waliipa ofa ya Pauni 40,000,001.
Ajabu Liverpool ilipiga chini ofa hiyo, lakini Suarez amesema walifanya kosa.
"Sifikirii kusalitiwa (na Liverpool) lakini klabu iliniahidi hivyo mwaka uliopita, kama nilivyowaahidi nitabaki kupigania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa,"amesema.
"Walinipa kauli hiyo mwaka uliopita, na sasa nawataka waheshimu hilo. Na si suala ambalo linamuhusu kocha, bali kitu fuani kilichoandikwa kwenye Mkataba. Siendi klabu nyingine ili kuiumiza Liverpool,"alisema.
John W Henry ameweka wazi kwamba Liverpool haina mpango wa kumuuza Suarez.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay atakosa mchezo wa kirafiki mjini Oslo dhidi ya Valerenga baada ya kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 21 cha Liverpool kwa sababu ya maumivu ya mguu.
Kocha Rodgers hakuwa na jinsi zaidi ya kumuacha Suarez baada ya kutolewa mazoezini mapema Melwood jana mchana, akishindwa kumaliza mazoezi ya kupasha misuli moto na kukimbia. Mara moja alipelekwa kufanyiwa vipimo.
Suarez amecheza mechi kadhaa za kujiandaa na msimu za Liverpool