• HABARI MPYA

    Friday, September 13, 2013

    BALAA GANI ARSENAL, OZIL HATIHATI KUCHEZA NA SUNDERLAND KESHO KWA SABABU MGONJWA

    IMEWEKWA SEPTEMBA 13, 2013 SAA 1:07 USIKU
    KOCHA Arsene Wenger anaweza kulazimika kuchelewa kuanza kumtumia Mesut Ozil baada ya kumsaini kwa Pauni Milioni 42baada ya kushindwa kufanya mazoezi leo kwa sababu anaumwa.
    Kocha huyo Arsenal ataamua mwishoni kabisa kama atamtumia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi.
    Ozil - kwa pamoja na Mjerumani mwenzake, Per Mertesacker - waliwasili makao makuu ya klabu, Colney, London asubuhi ya leo wakiwa wameathirika na hali ya hewa hivyo kuambiwa wasifanye mazoezi.
    Mchezaji huyo ghali wa Arsenal atasafiri na timu kwa ajili ya mechi na Sunderland, lakini madaktari wa timu wataangalia afya yake asubuhi ya kesho kama anaweza kumudu kucheza mechi hiyo.
    Sick for Sunderland? Ozil in training on Thursday before he was made to sit out
    Homa ya Sunderland? Ozil akifanya mazoezi jana kabla ya kutakiwa kupumzika
    Reaching for the title: Mesut Ozil and Per Mertesacker were all smiles earlier in the week before they both felt sick
    Mesut Ozil na Per Mertesacker

    Ikiwa hatacheza kesho, Ozil anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza kikamilifu Arsenal Jumatano katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Marseille au katika mchezo wa nyumbani wa Ligi Kuu na Stoke Jumamosi ijayo.
    Kiungo wa Czech, Tomas Rosicky pia ni majeruhi na ataukosa mchezo wa kesho kama ilivyo kwa mshambuliaji wa U21 ya Ufaransa, Yaya Sanogo, lakini wachezaji wawili wa England, Theo Walcott na Jack Wilshere wanatarajiwa kucheza pamoja na kiungo wa Wales, Aaron Ramsey.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BALAA GANI ARSENAL, OZIL HATIHATI KUCHEZA NA SUNDERLAND KESHO KWA SABABU MGONJWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top