IMEWEKWA SEPTEMBA 13, 2013 SAA 4: 52 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o amesema kwamba alikuwa anamchukia kocha Jose Mourinho kabla ya kuanza kufanya naye kazi Inter Milan.
Mourinho msimu wa 2009/2010 alitamba kwa kutwaa mataji matatu, na alifanya hivyo ya kumtumia Eto'o nje ya nafasi yake, akimchezesha pembeni kulia katika washambuliaji watatu alipomsajili kama mbadala wa Zlatan Ibrahimovic.
Na ni wakati huo Eto'o akifanya kazi na Mourinho Italia alipoanza kumpenda kocha hujyo Mreno lakini kabla ya hapo akiwa Barcelona wakati Mreno huyo akiifundisha Chelsea hakutaka kucheza chini yake.
Marafiki wameungana: Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Samuel Eto'o anafurahia kufanya kazi na Jose Mourinho tena
"Kabla ya kukutana naye Inter, tulikuwa hatufahamiani kila mtu, hivyo uhusiano wetu haukuwa mzuri," Eto'o aliiambia The Sun. "Niliwahi hadi kusema wakati mmoja kwamba sitakuja kucheza katika klabu ambayo Jose anaikochi.
"Lakini Mungu anafahamu vizuri. Alitaka kunionyesha kwamba nilikuwa napotoka na leo Jose ni rafiki. Leo ni kocha wangu tena,".
Mkali Eto'o amewasili Chelsea kwa uhamisho wa Pauni Milioni 7 kutoka Anzhi Makhachkala katika siku ya mwisho ya ya kufungwa kwa pazia la usajili, baada ya klabu hiyo kufeli kumsajili mchezaji iliyekuwa ikimtaka sana, Wayne Rooney.
Dole juu: Jose Mourinho hatimaye amempata mshambuliaji aliyemta, Eto'o amewasili
Kuna wakati Mcameroon huyo alipewa hila ya kuwa matatizo na ubinafasi na hilo lilichangia kuondoka kwake Barca mwaka 2009, lakini akiwabt Inter, chini ya Mourinho, mambo yaliendelea kumuendea vizuri.
Eto'o alihusishwa kwa kiasi kikubwa na kutua Chelsea mwaka 2006, wakati Adriano pia alipokuwa akitakiwa, kabla ya Andriy Shevchenko kusajiliwa kwa Pauni Milioni 30.
Historia itajirudia? Wawili hao walifanya mambo makubwa walipokuwa Italia na Inter Milan
Mataji matatu: Inter ilitwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa na mawili ya nyumbani msimu wa 2009/2010 wakati Mourinho akifanya kazi na Eto'o huko