• HABARI MPYA

    Friday, September 13, 2013

    MRISHO KHALFAN NGASSA 'SI MZIMA, HUU NI WAZIMU'...

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA SEPTEMBA 13, 2013 SAA 2:04 ASUBUHI
    ANA ‘wazimu’ wa magari. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu ‘Young Don’ Mrisho Khalfan Ngassa, baada ya kutoa Sh. Milioni 21 kununua gari mpya aina ya Peugeot.
    Sasa Ngassa anakuwa na gari 10, kati ya hizo kuna mbili alizowapa wazazi wake, baba na mama yake moja ya familia na tatu za kibiashara.
    Mkoko mpya wa Young Don; Gari jipya la Mrisho Khalfan Ngassa


    Ngassa katika gari lake jipya 

    Kwa sasa, Ngassa ameiambia BIN ZUBEIRY atakuwa anatumia zaidi ‘mkoko’ wake mpya badala ya ile Nissan ambayo amekuwa akionekana nayo siku za karibuni.
    Wakati fulani, alionekana na Prado kwenye mazoezi ya Yanga na kuhusu gari hilo, Ngassa anasema; “Halikuwa gari langu lile, kuna mjomba wangu alichukua gari langu akaniachia lile la kwake,”alisema.  
    Kwa sasa Ngassa yuko Mwanza alipokwenda kuhudhuria mazishi ya bibi yake mzaa baba, Bi Joha aliyefariki dunia mapema wiki hii.  
    Magari ya Ngassa yamepagana nyumbani kwake


    Ni gari kali

    Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa ‘Babu’ anatarajiwa kupanda ndege leo mjini Mwanza kwenda Mbeya kuungana na timu yake, Yanga SC ambayo ipo huko kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Mbeya City kesho.
    Hata hivyo, Ngassa kwa sasa hachezi kutokana na kuwa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi sita na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusaini timu mbili, Simba na Yanga SC. Tayari amekosa mechi tatu.
    Ngassa kwenye mazishi ya bibi yake

    Ngassa ametakiwa arejeshe fedha za Simba SC Sh. Milioni 30 na kulipa fidia ya Sh. Milioni 15 ndipo aruhusiwe kuchezea Yanga SC.  
    Kama Yanga SC itawahi kumlipia faini hiyo Ngassa, anaweza kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu arejee kutoka Simba SC katika mchezo na Ruvu Shooting Septemba 28, maana yake atakosa pia mechi na Azam Septemba 22 ambayo itakuwa ya sita.
    Baada ya mchezo wa kesho, Yanga itabaki Mbeya kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Jumatano dhidi ya Prisons. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MRISHO KHALFAN NGASSA 'SI MZIMA, HUU NI WAZIMU'... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top