Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA SEPTEMBA 13, 2013 SAA 1:56 ASUBUHI
AZAM FC leo inatarajiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kabla ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Azam iliyofika Kagera jana asubuhi kwa ndege, imeweka kambi yake katika hoteli ya Smart, iliyopo maeneo ya Nyamkazi mkoani humo.
Washindi hao wa pili mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu, jana walifanya mazoezi yao ya kwanza mkoani humo kwenye Uwanja wa Ntungamo.
Huo utakuwa mchezo wa tatu wa Ligi Kuu kwa Azam msimu huu, baada ya awali kutoa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Manungu mkoani Morogoro kabla ya kushinda 2-0 dhidi ya Rhino Rangers mkoani Tabora.
Kagera yenyewe itakuwa ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa nyumbani msimu huu, baada ya awali kutoka 0-0 na Mbeya City mjini Mbeya na kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar Manungu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu kesho ni kati ya Mbeya City na Yanga Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Simba SC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Coastal Union na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shootings na Mgambo JKT (Mabatini, Pwani), JKT Oljoro na Rhino Rangers (Sheikh Amri Abeid, Arusha) na Ashanti United na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Macho na masikio ya wengi yatakuwa katika mechi za vigogo Simba na Yanga hiyo kesho.
Yanga itakuwa inacheza kwa mara ya kwanza ugenini, baada ya awali kucheza mechi mbili mfululizo nyumbani na kuvuna pointi nne, kutokana na ushindi wa 5-1 dhidi ya Ashanti United na sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union.
Ni kama watani wao tu Simba SC, watakuwa wakicheza nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya awali kuvuna pointi nne ugenini kwa sare ya 2-2 na Rhino Rangers mjini Tabora na ushindi wa 1-0 na JKT Oljoro mjini Arusha.
Lakini pia Wagosi wa Kaya, Coastal Union waliosajili vizuri mno msimu huu pengine kuliko timu nyingine yoyote nao watamulikwa pale Mkwakwani, baada ya awali kuvuna pointi nne ugenini, kwa ushindi wa 2-0 Arusha mbele ya JKT Oljoro na sare ya 1-1 na Yanga Dar es Salaam.
Kwa ujumla mechi hizi za tatu za Ligi Kuu zinatarajiwa kutoa picha halisi ya kila timu na hivyo kujua washindani ni akina nani na wasindikizaji ni akina nani. (Angalia matokeo ya mechi zote za awali na Ratiba nzima ya mzunguko wa kwanza upende wa kulia wa ukurasa).

![]() |
Wapo Kagera; Azam leo watashuka dimbani uwanja wa Kaitaba kufanya mazoezi kabla ya mechi kesho dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar |
Huo utakuwa mchezo wa tatu wa Ligi Kuu kwa Azam msimu huu, baada ya awali kutoa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar Manungu mkoani Morogoro kabla ya kushinda 2-0 dhidi ya Rhino Rangers mkoani Tabora.
Kagera yenyewe itakuwa ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa nyumbani msimu huu, baada ya awali kutoka 0-0 na Mbeya City mjini Mbeya na kufungwa 1-0 na Mtibwa Sugar Manungu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu kesho ni kati ya Mbeya City na Yanga Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Simba SC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Coastal Union na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shootings na Mgambo JKT (Mabatini, Pwani), JKT Oljoro na Rhino Rangers (Sheikh Amri Abeid, Arusha) na Ashanti United na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
![]() |
Wanaanza kazi viwanja vibovu; Yanga SC watakuwa Mbeya kesho |
Macho na masikio ya wengi yatakuwa katika mechi za vigogo Simba na Yanga hiyo kesho.
Yanga itakuwa inacheza kwa mara ya kwanza ugenini, baada ya awali kucheza mechi mbili mfululizo nyumbani na kuvuna pointi nne, kutokana na ushindi wa 5-1 dhidi ya Ashanti United na sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union.
Ni kama watani wao tu Simba SC, watakuwa wakicheza nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya awali kuvuna pointi nne ugenini kwa sare ya 2-2 na Rhino Rangers mjini Tabora na ushindi wa 1-0 na JKT Oljoro mjini Arusha.
Lakini pia Wagosi wa Kaya, Coastal Union waliosajili vizuri mno msimu huu pengine kuliko timu nyingine yoyote nao watamulikwa pale Mkwakwani, baada ya awali kuvuna pointi nne ugenini, kwa ushindi wa 2-0 Arusha mbele ya JKT Oljoro na sare ya 1-1 na Yanga Dar es Salaam.
![]() |
Wamerudi nyumbani; Simba SC watakuwa Taifa kesho |