Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 10, 2013 SAA 3:50 ASUBUHI
WAKATI majeruhi wa muda mrefu wa Azam FC, beki Mzanzibari Samih Hajji Nuhu, kiungo Mkenya Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony wameanza mazoezi ya gym baada ya kuweka chini magongo, majeruhi mwingine wa timu hiyo, mshambuliaji mzawa, John Bocco anaendelea vizuri.
Habari njema zaidi kwa wapenzi wa Azam FC ni kwamba, kiungo tegemeo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo, amepona na jana ameanza mazoezi.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kwa ujumla majeruhi wote wanaendelea vizuri na Sure Boy amepona kabisa.
Hata hivyo, Jemadari amesema hakuna kati yao Nuhu, Mieno, Umony na Bocco atakayeweza kusafiri na timu kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar.
“Hajji, Mieno na Umony wanaweza kuanza mazoezi wiki ijayo, ila kwa sasa wanafanya mazoezi ya gym. Na kwa Bocco yeye anasumbuliwa na maumivu ya nyama tu, ambayo kupona yatategemea ugumu wake, ila si maumivu ya kutisha na hatutarajii kumkosa kwa muda mrefu,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Kariakoo United ya Lindi.
Hajji, Mieno na Umony waliuamia mwanzoni mwa mwaka katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, wakati Bocco aliumia mwezi uliopita katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC, Dar es Salaam.
Sure Boy alimaliza dakika 90 katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu wa Azam mjini Tabora dhidi ya wenyeji Rhino Rangers na usiku wake akashikwa na tumbo la kuendesha ambalo lilimsababishia homa pia.
Kwa sababu hiyo, wote Bocco na Sure Boy wakashindwa kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichomenyana na Gambia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Makundi kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Azam inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam na kesho wachezaji wote wataingia kambini tayari kwa safari ya Bukoba Alhamisi asubuhi.
Kwa sababu Bocco bado majeruhi, safu ya ushambuliaji ya Azam itaendelea kuongozwa na Gaudence Mwaikimba na Kipre Tchetche katika mchezo dhidi ya Kagera, ambao mmoja wao baadaye anaweza kumpisha Seif Abdallah Karihe.
Kocha Muingereza, Stewart Hall alitarajiwa kurejea jana kutoka kwao Uingereza alipokwenda kwa matibabu baada ya mechi na Rhino wiki iliyopita na kipindi chote hiki timu imekuwa chini ya kocha Msaidizi, Kali Ongala.
WAKATI majeruhi wa muda mrefu wa Azam FC, beki Mzanzibari Samih Hajji Nuhu, kiungo Mkenya Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony wameanza mazoezi ya gym baada ya kuweka chini magongo, majeruhi mwingine wa timu hiyo, mshambuliaji mzawa, John Bocco anaendelea vizuri.
Habari njema zaidi kwa wapenzi wa Azam FC ni kwamba, kiungo tegemeo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo, amepona na jana ameanza mazoezi.
![]() |
| Karibu kurejea; Brian Umony kushoto ameanza mazoezi ya gym. Kulia ni Kipre Tchetche yuko fiti na atacheza Bukoba |
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kwa ujumla majeruhi wote wanaendelea vizuri na Sure Boy amepona kabisa.
Hata hivyo, Jemadari amesema hakuna kati yao Nuhu, Mieno, Umony na Bocco atakayeweza kusafiri na timu kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa wiki dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar.
“Hajji, Mieno na Umony wanaweza kuanza mazoezi wiki ijayo, ila kwa sasa wanafanya mazoezi ya gym. Na kwa Bocco yeye anasumbuliwa na maumivu ya nyama tu, ambayo kupona yatategemea ugumu wake, ila si maumivu ya kutisha na hatutarajii kumkosa kwa muda mrefu,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Kariakoo United ya Lindi.
![]() |
| Bado bado; John Bocco bado anasumbuliwa na maumivu. Khamis Mcha 'Vialli' kulia yuko fiti na atakwenda Bukoba |
Sure Boy alimaliza dakika 90 katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu wa Azam mjini Tabora dhidi ya wenyeji Rhino Rangers na usiku wake akashikwa na tumbo la kuendesha ambalo lilimsababishia homa pia.
Kwa sababu hiyo, wote Bocco na Sure Boy wakashindwa kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichomenyana na Gambia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Makundi kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Azam inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam na kesho wachezaji wote wataingia kambini tayari kwa safari ya Bukoba Alhamisi asubuhi.
![]() |
| Gaudence Mwaikimba ataendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Azam Bukoba |

.png)