• HABARI MPYA

    Tuesday, September 10, 2013

    BARCELONA YALAMBA UDHAMINI MPYA MNONO WA MABILIONEA WA KIARABU

    Na Nurat Mahmoud, IMEWEKWA SEPTEMBA 10, 2013, SAA 3:00 ASUBUHI
    KLABU ya Barcelona imeingia Mkataba wa miaka mitatu wa udhamini na Benki ya Umoja wa Arabuni (UAB), ambayo inaelezwa mabingwa hao wa La Liga wanakuwa klabu ya kwanza ya soka kuingia ushirika na benki hiyo ya Falme za Kiarabu (UAE).
    Udhamini mpya huu hapa

    Barca haijaweka wazi taarifa za makubaliano ya fedha za udhamini huo, ambao utakwenda hadi Julai 2016, lakini imeelezewa wateja wa UAB watakuwa wanazawadiwa "siti za vibosile" kuangalia mechi za klabu hiyo.
    "Benki ya Umoja wa Arabuni inatazamia kuwapa faraja wateja wake wapendano soka na FC Barcelona kwa ujumla," Barca imesema katika taarifa yake kwenye tovuti yake (www.fcbarcelona.es).
    "Kama wadhamini rasmi wa klabu, itautumia uhusiano huu na Barca kuwa na bidhaa ambazo zitawafurahisha mashabiki wengi wa Barca UAE."
    Benki ya Umoja wa Arabuni (UAB), ni taasisi ya kifedha inayokuwa kwa kasi UAE, na imetangaza kuungia ushirika na moja ya klabu kubwa duniani, FC Barcelona.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCELONA YALAMBA UDHAMINI MPYA MNONO WA MABILIONEA WA KIARABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top