IMEWEKWA SEPTEMBA 9, 2013 SAA 1:05 USIKU
NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas amemtabiria mchezaji mpya wa Gunners, Mesut Ozil kutikisa katika Ligi Kuu ya England.
Fabregas aliondoka klabu hiyo Kaskazini mwa London kuhamia Barcelona mwaka 2011, lakini bado ana ukaribu klabu hiyo.
Anaamini mchezaji huyo nyota wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 atang'ara katika Ligi Kuu ya England.
Niamini: Kiungo wa Barca, Cesc Fabregas (juu) anataraji mchezaji mpya wa Arsenal, Mesut Ozil (chini) atang'ara England
Akizungumza na Al Primer Toque, Fabregas alisema: "Anakwenda kufurahia katika Ligi Kuu England tena sana tu. Ni ligi yenye nafasi zaidi na Ozil ni mchezaji wa aina hiyo, ukimpa muda na nafasi, anakuua. Kama ambavyo tumeona wakati akiwa Real Madrid, mpira wake wa mwisho ni hatari na naamini kwamba atafurahia England,"amesema. Ozil anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza The Gunners dhidi ya Sunderland Uwanja wa Light Jumamosi.
Uzoefu: Fabregas alijiunga na The Gunners akiwa na umri wa miaka 16 anafahamu sana kuhusu Ligi Kuu ya England.


.png)