Na Princess Asia, IMEWEKWA SEPTEMBA 8, 2013 SAA 7:10 USIKU
BAO la kiungo Sadio Mane wa Senegal dakika ya 84, usiku huu limeizamisha Uganda 1-0 kwenye Uwanja wa Marrakech mjini Marrakech, Morocco katika mchezo wa mwisho kabisa wa hatua ya makundi kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Hata hivyo, Uganda iliathiriwa na kadi nyekundu ya mapema aliyopewa mchezaji wake Godfrey Walusimbi dakika ya 34 na kucheza pungufu tangu hapo.
Matokeo hayo yanazima ndoto za Uganda kuingia hatua ya mwisho ya mbio za Brazil mwakani, baada ya kuiacha Senegal iongoze Kundi J kwa kufikisha pointi 12.
Uganda inayofundishwa na Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ inabaki na pointi zake nane baada ya matokeo hayo na ingesonga mbele kama ingeshinda mechi hiyo.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emanuel Okwi alicheza kwa dakika 84 kabla ya kumpisha Kalanda.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza alicheza kwa dakika 81 kabla ya kumpisha Kayongo Mutumba.
Mshambuliaji anayewaniwa na timu zote, Simba na Yanga, Moses Oloya alitokea benchi dakika ya 59 kwenda kuchukua nafasi ya Godfrey Kizito, lakini hakuiepusha Uganda na kipigo.
Kikosi cha Senegal kilikuwa; B. Coundoul, L. Gassama, C. Kouyate, P. Djilobodji, I. Cissokho, M. Diame, I. Gueye, S. Mane, S. Badji, H. Saivet na M. Diouf.
Uganda; Robert Odongokara, Andy Mwesigwa, Godfrey Walusimbi, Isaac Isinde, Dennis Iguma, Hassan Wasswa, Godfrey Kizito/Moses Oloya dk59, Brian Majwega, Tonny Mawejje, Hamisi Kiiza/Kayongo Mutumba dk81 na Emanuel Okwi/Kalanda dk 84.
BAO la kiungo Sadio Mane wa Senegal dakika ya 84, usiku huu limeizamisha Uganda 1-0 kwenye Uwanja wa Marrakech mjini Marrakech, Morocco katika mchezo wa mwisho kabisa wa hatua ya makundi kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Hata hivyo, Uganda iliathiriwa na kadi nyekundu ya mapema aliyopewa mchezaji wake Godfrey Walusimbi dakika ya 34 na kucheza pungufu tangu hapo.
![]() |
| Okwi ameshindwa kuisaidia Uganda |
Matokeo hayo yanazima ndoto za Uganda kuingia hatua ya mwisho ya mbio za Brazil mwakani, baada ya kuiacha Senegal iongoze Kundi J kwa kufikisha pointi 12.
Uganda inayofundishwa na Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ inabaki na pointi zake nane baada ya matokeo hayo na ingesonga mbele kama ingeshinda mechi hiyo.
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emanuel Okwi alicheza kwa dakika 84 kabla ya kumpisha Kalanda.
![]() |
| Kiiza ameshindwa kuibeba Uganda |
Mshambuliaji anayewaniwa na timu zote, Simba na Yanga, Moses Oloya alitokea benchi dakika ya 59 kwenda kuchukua nafasi ya Godfrey Kizito, lakini hakuiepusha Uganda na kipigo.
![]() |
| Oloya aliingia dakika ya 59, lakini nakachemsha pia |

.png)