IMEWEKWA SEPTEMBA 12, 2013 SAA 5:35 USIKU
MCHEZAJI mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil amekiri Ligi Kuu ya England ni ya miguvu lakini hana anachohofia na yuko tayari kuendana na mchezo huo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24 alisema hayo baada ya mazoezi yake ya kwanza na timu hiyo asubuhi ya leo, tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid.
"Naangalia mbele kucheza ligi hii, nimeangalia mechi nyingi za Ligi Kuu," alisema Ozil. "Kweli, ni soka ya miguvu sana, ni mchezo wa watu, na ninataka kujidhihirisha England. Pia nimecheza Bundesliga na Hispania na kujidhihirisha,".
VIDEO Kaangalia Mesut Ozil akisema: Mimi ni Mtutu!
Maskani mpya: Mesut Ozil amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Arsenal tangu asajiliwe kutoka Real Madrid
Karibu England: Beki wa Arsenal, Per Mertesacker (kushoto) akifanya mazoezi na Mjerumani mwenzake, Mesut Ozil
Ozil pia alizungumzia sababu za kutosikitika kuondoka Madrid ni kutokana na kocha Arsene Wenger kujenga imani kubwa juu yake na hiyo ndiyo ilimfanya akubali kuhamia Arsenal, kwani nayo ni klabu kubwa duniani.
Hakuna kuangalia nyuma: Ozil akiwa mwenye raha katika mazoezi yake ya kwanza Arsenal
Mchezaji ghali: Ozil amejiunga Arsenal kutoka Real Madrid kwa Pauni Milioni 42
Poa kabisa: Ozil akijifua mazoezini Arsenal