Na Prince Akbar, Banjul, Gambia IMEWEKWA SEPTEMBA 7, 2013 SAA 3:40 USIKU
TANZANIA, Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Gambia usiku huu kwenye Uwanja wa Independence mjini Banjul katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kuhitimisha hatua ya awali ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Kwa matokeo hayo, Stars imemaliza na pointi sita katika nafasi ya tatu, nyuma ya Morocco wa pili pointi tisa na Ivory Coast vinara wa kundi pointi 14, wakati Gambia wameshika mkia kwa pointi zao nne, huu wa leo ukiwa ushindi wao pekee kwenye kundi hilo.
Mbaya wa Stars leo alikuwa ni mshambuliaji Mustapha Alasan Jarju mwenye umri wa miaka 27 aliyefunga katika dakika ya 45 na 51 mabao yote hayo.
Mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Morocco na Tembo wa Ivory Coast kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, umeisha kwa sare ya 1-1 bao la Simba wa Atlasi lilkifungwa na Youssef El-Arabi dakika ya 53 na Didier Drogba akawasawazishia Tembo dakika ya 83.
Matokeo haya yanaamisha kufeli vibaya kocha Mdenmark, Kim Pouslen baada ya awali Tanzania kukosa tiketi za kucheza Fainali za AFCON na CHAN chini yake.
Kim alirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen Mei mwaka jana na leo ulikuwa mchezo wake wa 16 kazini, akifungwa saba, sare nne na kushinda mitano.
Kikosi cha Gambia kilikuwa; B. Sanyang, A. Mansally, O. Colley, S. Marreh, T. Jaiteh, E. Sohna, H. Barry, S. Faal, M. Jarju na M. Ceesay.
Stars; Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni/David Luhende dk70, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha/Juma Liuzio dk61.

![]() |
| Mbaya wetu; Mustafa Jaju amefunga mabao yote ya Gambia |
Kwa matokeo hayo, Stars imemaliza na pointi sita katika nafasi ya tatu, nyuma ya Morocco wa pili pointi tisa na Ivory Coast vinara wa kundi pointi 14, wakati Gambia wameshika mkia kwa pointi zao nne, huu wa leo ukiwa ushindi wao pekee kwenye kundi hilo.
![]() |
| Stars imechapwa 2-0 Gambia leo |
Mbaya wa Stars leo alikuwa ni mshambuliaji Mustapha Alasan Jarju mwenye umri wa miaka 27 aliyefunga katika dakika ya 45 na 51 mabao yote hayo.
Mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Morocco na Tembo wa Ivory Coast kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, umeisha kwa sare ya 1-1 bao la Simba wa Atlasi lilkifungwa na Youssef El-Arabi dakika ya 53 na Didier Drogba akawasawazishia Tembo dakika ya 83.
![]() |
| Amechemsha; Stars imeshindwa kupata mafanikio chini ya Kim Poulsen |

.png)