• HABARI MPYA

    Wednesday, September 11, 2013

    YANGA SC TAYARI WAKO NJIANI KUELEKEA MBEYA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 11, 2013 SAA 2:04 ASUBUHI
    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wameondoka leo asubuhi kwa basi lao kwenda Mbeya tayari kwa michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Jumamosi dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine mjini humo. 
    Baada ya Jumamosi kucheza na timu hiyo mpya katika Ligi Kuu, Yanga watateremka tena dimbani Jumatano kumenyana na Prisons kwenye Uwanja huo huo. 
    Yanga SC

    Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Ernie Brandts ameondoka na kikosi chake akiwa na matumaini makubwa ya ushindi Mbeya, ili kutimiza ndoto za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.
    Wachezaji walioondoka na timu ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Yusuph Abdul, mabeki Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Rajab Zahir, Ibrahim Job na Issa Ngao.
    Viungo ni Athuman Idd ‘Chuji’, Salum Telela, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani, Hamisi Thabit na Bakari Masoud, wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Abdallah Mguhi, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Shaban Kondo na Reliants Lusajo.
    Tayari Yanga SC imecheza mechi mbili nyumbani na kushinda moja dhidi ya Ashanti United 5-1 kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SC TAYARI WAKO NJIANI KUELEKEA MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top