• HABARI MPYA

    Thursday, September 12, 2013

    YANGA SC YAMTANGAZA RASMI NAGGI

    Na Princess Asia, IMEWEKWA SEPTEMBA 12, 2013 SAA 7:35 MCHANA
    KLABU ya Yanga SC imetangaza rasmi kumuajiri Mkenya, Patrick Naggi, na watu wengine wawili, ingawa imesema Lawrence Mwalusako ataendelea kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa klabu.
    Naggi

    Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga amesema kwamba uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana mjini Dar es Salaam.
    Sanga amewaambia Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba Naggi ameajiriwa katika uongozi wa Yanga pamoja na Beno Salvatory Njovu (Mshauri wa Mambo ya Utawala na Fedha) na George Simba Magani atakayefanya shughuli za masoko.
    Sanga amesema kwamba waajiriwa wote hao wapya, nafasi zao rasmi zitatangazwa baada ya miezi miwili, wakati Mwalusako anaendelea kukaimu Ukatibu, wakati mchakato wa ajira rasmi ya nafasi yake unaendelea.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SC YAMTANGAZA RASMI NAGGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top