Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA SEPTEMBA 12, 2013 SAA 12:16 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Ally Hafidh Badru amesajiliwa na Azam FC kutoka Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imefahamika.
Badru alisajiliwa mapema tu, lakini Azam ilichelewa kuweka bayana usajili wake, kwa kuwa ilikuwa inasubiri barua ya klabu yake, Suez kuthibitisha kwamba ilimruhusu kuondoka.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Badru kipenzi cha kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hafidh Badru alisema kwamba barua tayari imefika.
“Barua imefika, na ilichelewa kufika kwa sababu Misri kwa sasa kuna machafuko. Ila sasa imefika kwa hiyo wakati wowote nitajiunga na Azam kuanza kazi,”alisema.
Alipoulizwa sababu za kuondoka Misri na kurejea Tanzania, Badru alisema kwa sasa Ligi hazichezwi nchini humo na haijulikani zitaanza lini kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea.
“Nilijiunga na timu hiyo miaka mitatu iliyopita kwa Mkataba wa miaka mitano na hadi naondoka nilikuwa nimebakiza miaka miwili. Ila mimi na wachezaji wengine wote wa kigeni, tuliambiwa tukipata timu tuondoke kwa saabu hali kule haijulikani itatulia lini,”.
“Sasa baada ya kuja na kusaini Azam mapema tu kabla ya dirisha halijafungwa na jina langu kupelekwa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), Azam wakasema wanasubiri barua ya Canal Suez kuthibitisha wameniruhusu kuondoka,”.
“Ilikuwa tabu kidogo kupatikana hiyo barua kutokana na vurugu zinazoendelea kule (Misri), hatimaye jana (juzi) hiyo barua imefika na nimewasiliana na Azam ili niwapelekee, kwa hiyo wakati wowote nitakutana na Azam ili kuwapa hiyo barua,”alisema.
Badru atakuwa mchezaji pekee kusajiliwa na Azam msimu huu na anakuja katika wakati mwafaka, klabu hiyo ikikabiliwa na majeruhi wengi katika safu yake ya ushambuliaji.
Kiungo mshambuliaji Mkenya Humphrey Mieno, washambuliaji Mganda, Brian Umony na mzawa John Bocco ‘Adebayor’ wote ni majeruhi kwa sasa na Azam inabaki na washambuliaji watatu tu, Kipre Tchetche ambaye kwa sasa anacheza pembeni na Gaudence Mwaikimba na chipukizi Seif Abdallah.

![]() |
Kifaa kweli; Badru Hafidh Ally ametua Azam |

Anaweza; Badru akiwatoka wachezaji wawili wa Burundi akiichezea Zanzibar Kombe Challenge mwaka 2011 |
![]() |
Ana nguvu na kasi; Badru akimtoka beki Kaze Gilbert wa Burundi katika Challenge ya 2011 Dar es Salaam |