• HABARI MPYA

    Thursday, September 12, 2013

    HABARI NJEMA MAN UNITED, ROONEY AREJEA KAZINI..AANZA MAZOEZI RASMI, NA FELLAINI...

    IMEWEKWA SEPTEMBA 12, 2013 SAA 12:10 ASUBUHI
    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney yuko tayari kuanza mazoezi kamili na Manchester United akidhamiria kuwa kujiweka fiti kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu, City Jumapili.
    Rooney, mwenye umri wa miaka 27, alikuwa akifanya mazoezi na wataalamu wa tiba wa United kwenye Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington jana na anaonekana kuwa fiti baada ya kuumia kichwa alipogongana na Phil Jones kiasi cha wiki mbili zilizopita.
    Lakini mshambuliaji huyo United anapewea asilimia 50 kwa 50 kucheza mechi dhidi ya timu ya Manuel Pellegrini, City Uwanja wa Etihad, Septemba 22.
    On the mend: Wayne Rooney poses with a fan after recovering from his head injury - he was back in training for the first time on Wednesday
    Kipenzi cha mashabiki: Wayne Rooney akipiga picha na shabiki baada ya kupona maumivu ya kichwa na kuanza mazoezi jana
    Nasty: Wayne Rooney's head injury kept him out of England's matches but he is now back in training
    Jeraha: Wayne Rooney' alivyoumia kichwani kiasi cha kushindwa kuitumikia England, ila sasa amerejea mazoezini
    R and R: Rooney spent the international break on holiday in the Algarve
    R na R: Rooney alikuwa mapumzikoni Algarve
    Wary: Rooney is understood to be training on his own away from the first team squad, with David Moyes not willing to rush him back into action
    Wasiwasi: Rooney inafahamika alikuwa anafanya mazoezi kivyake nje ya timu, na David Moyes hayuko tayari kumharakisha kurejea uwanjani

    Moyes tayari amekubali kumkosa Rooney katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace Ligi Kuu ya England na anatarajiwa kucheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayer Leverkusen Uwanja wa Old Trafford JUmanne ijayo.
    Mchezaji mkubwa pekee aliyesainiwa United ni Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 25, na anatarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa wiki hii.
    Mshambuliaji huyo amecheza kikamilifu mechi moja tu United msimu huu, na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika sare ya 0-0 na Chelsea Uwanja wa Old Trafford. 
    Alitokea benchi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Swansea, akitoa mchango wa kupatikana mabao mawili kati ya manne ambayo timu yake ilivuna siku hiyo.
    Prepared: Marouane Fellaini has taken part in his first United training session and is in line to make his debut
    Anajiandaa: Marouane Fellaini amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza United na anatarajiwa kuanza kazi
    50/50: Rooney may well return for the Manchester derby on September 22
    50/50: Rooney anaweza kurejea katika mechi dhidi ya wapinzani wa Jiji la Manchester, Septemba 22
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HABARI NJEMA MAN UNITED, ROONEY AREJEA KAZINI..AANZA MAZOEZI RASMI, NA FELLAINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top