IMEWEKWA SEPTEMBA 12, 2013 SAA 11:57 ALFAJIRI
KIUNGO Mesut Ozil amewasili katika klabu yake mpya jana, Arsenal tayari kuanza kumtumikia Arsene Wenger anayekabiliwa na tatizo la wachezaji wengi majeruhi.
Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42 ataanza mazoezi leo makao makuu ya klabu, Colney London kwa mara ya kwanza tangu ahamie akitokea Real Madrid.
Na Wenger anajiandaa kumtumia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika mchezo dhidi ya Sunderland Jumamosi baada ya Tomas Rosicky kurejea kwenye mechi ya timu yake ya taifa akiwa majeruhi.
Tayari marafiki? Alex Oxlade-Chamberlain ni miongoni mwa wachezaji wa awali wa Arsenal kukutana na Mesut Ozil
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech aliumia wakati timu yake ikilala 2-1 dhidi ya Italia na yuko shakani kucheza Uwanja wa Light.
Hiyo inaacha milango wazi mno kwa Ozil kuanza kazi Arsenal, licha ya kwanza atakuwa na siku mbili tu kamili za kufanya mazoezi na wenzake kabla ya mechi hiyo.
Licha ya msimu kuwa umekwishaanza kwa karibu mwezi mzima, Arsenal tayari ina idadi kubwa ya majeruhi.
Kifaa kipya, ofisi mpya: Ozil amepigwa pichwa makao makuu wa Arsenal, kwenye viwanja vya mazoezi vya Colney London kwa mara ya kwanza
Wa nchi moja, klabu moja: Lukas Podolski na Ozil tayari wamekuwa wakicheza pamoja timu ya taifa ya Ujerumani
Mwendeshaji hodari: Ozil alidhihirisha tena uwezo wake alipoiongoza Ujerumani kuilaza 3-0 Faroe Islands
Rosicky anaungana na Thomas Vermaelen, Mikel Arteta, Alex Oxlade-Chamberlain, Lukas Podolski, Abou Diaby na Yaya Sanogo katika chumba cha majeruhi wa klabu hiyo.
Habari njema kwa Wenger ni kwamba, Theo Walcott na Jack Wilshere wanatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo wa Jumamosi baada ya kushindwa kuichezea England mjini Kiev.
Wilshere alitolewa katikati ya kipindi cha pili na Walcott alitolewa baada ya kuumia akipambana na Oleksandr Kucher.
Lakini wote wanatarajiwa kucheza dhidi ya timu ya Paolo Di Canio mwishoni mwa wiki hii.